TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Tuesday, December 1, 2009

Babu Seya tena kortini

2:38 PM

Hatimaye mwanamuziki Nguza Vicking almaarufu kama Babu Seya na wanawe watatu, leo wametinga kortini tena katika Mahakama ya Rufaa Jijini kwa nia ya kupinga adhabu waliyo nayo sasa ya kutumikia kifungo cha maisha.

Rufaa ya Nguza na wanawe hao ambao ni Nguza Machine, Papii Nguza na Francis Nguza imeanza kusikilizwa leo na jopo la majaji watatu wa Mahakama hiyo ya Rufaa, ambao ni Jaji Nathalia Kimaro, Mbarouk Mbarouk na Salum Massati.

Aidha, wakili wa upande wa walalamikaji katika kesi hiyo ni Bw. Mabere Marando.

Nguza na wanawe ambao walihukumiwa kifungo cha maisha kutokana na kukutwa na hatia katika kesi ya kuwaingilia watoto 10 wa Shule ya Msingi Mashujaa iliyopo Sinza Jijini, walifika mahakamani hapo mapema leo asubuhi.

Nguza alionekana akiwa amevalia vazi lenye muonekano wa mavazi ya Kinijeria huku mwanawe Papii akiwa amevalia rozali yake shingoni.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA