TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Wednesday, December 30, 2009

Asakwa kwa kumnyonga rafikiye chumbani

3:28 PM
Jeshi la polisi mkoani Ruvuma linamsaka kijana mmoja kwa tuhuma za kumuua rafiki yake waliokuwa wakiishi naye chumba kimoja kwa sababu ambazo hazijafahamika na kisha kukimbia.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda, aliiambia Nipashe kwa njia ya simu kuwa tukio hilo lilijiri Desemba 28 mwaka huu, saa 3:30 asubuhi katika mtaa wa Majengo mjini Songea.
Alisema katika tukio hilo, kijana wa miaka 20, Rashidi Yasin, anadaiwa kumuua rafiki yake, alimtaja kwa jina moja, Abdalah (20) kwa kumkaba shingoni hadi kumsababishia kifo.
Akisimulia, Kamanda Kamhanda alisema kuwa vijana hao ambao walikuwa wakiishi katika chumba kimoja mjini hapa, siku ya tukio walitokea kwenye mahangaiko yao na kuingia kwenye chumba walichopanga.
“Baada ya muda, mtuhumiwa, Rashid, alionekana akivunja dirisha na kuruka, kisha akatimua mbio huku akiangua kilio, hali iliyowashitua wapangaji wengine,” alisema.
Alisema kuwa wapangaji hao waliamua kufungua mlango wa chumba hicho ndipo walipomkuta Abdallah akiwa ameshakufa.
Akimakariri mmoja wa wapangaji wa nyumba hiyo, Kamanda Kamuhanda alisema vijana hao marafiki na walipanga katika nyumba hiyo wakitokea wilayani Tunduru kwa kile walichodai kuwa wamekuja mjini Songea kutafuta maisha na kwamba walikuwa wakijihusisha na biashara ya kuuza bidhaa mbali mbali za urembo kwa kutembeza mitaani.
Alisema polisi wanaendelea kumsaka mtuhumiwa ambaye mapaka sasa haijulikani alikokimbilia.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA