TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Saturday, November 7, 2009

Mzinifu apigwa mawe hadi kufa Somalia

12:29 AM

Wanamgambo kusini mwa Somalia, wamempiga mawe hadi kufa mwanaume mmoja aliyekiri mbele ya mahakama ya kiisilamu kuwa mzinifu.

Hata hivyo mpenzi wa mwanaume huyo alinusurika kifo kwa kuwa ni mja mzito.

Abas Hussein Abdirahman, mwenye umri wa miaka 33, aliuawa mbele ya umati wa watu takriban miatatu katika mji wa bandari wa Merka.

Afisaa mmoja wa kundi la al-Shabab amesema kuwa mwanamke huyo atauawa baada ya kujifungua mwanawe.

Makundi ya wapiganaji yanadhibiti maeneo ya kusini mwa Somalia huku serikali ya mpti ikiwa na udhibiti wa sehemu za mji mkuu Mogadishu.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA