TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Wednesday, November 4, 2009

Mkurugenzi awatisha wafanyakazi waliokuwa Necta

1:42 PM

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Edmund Kinwasi, ametishia kuwafukuza kazi wafanyakazi zaidi ya 70 waliokuwa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) baada ya kwenda kudai malipo ya mishahara yao ya Septemba na Oktoba ambayo hawajalipwa hadi sasa.

Wafanyakazi hao ni wale waliohamishwa kutoka Necta na kupelekwa mikoa mbalimbali nchini, Julai mwaka huu.

Wafanyakazi hao ambao wanatoka mikoa mbalimbali walikusanyika wizarani kutaka kuonana na Mkurugenzi huyo ili kujua sababu zilizopelekea kuchelewa kwa mishahara yao kwa miezi miwili. Awali, wafanyakazi hao waliomba Mkurugenzi huyo atoke nje ili aweze kuzungumza nao kwa pamoja lakini aligoma na kutaka wafanyakazi wawili waingie ofisini kwake kwa ajili ya kuwawakilisha wenzao.

Pendekezo la Kinwasi lilikubaliwa na wafanyakazi hao ambapo waliwachagua wenzao wawili kwenda kuzungumza naye wakiwa na Katibu wa Chama Cha Wafanyakazi (Tughe), Omary Mkali.

Hata hivyo, wafanyakazi hao walipoingia tu ndani ya ofisi, Mkurugenzi huyo aliwakaripia na kusema "kumbe ni ninyi, matatizo yenu yanashughulikiwa, sihitaji hata kuwaona."

Kauli hiyo iliwalazimu wafanyakazi kumwomba kumweleza japo kwa dakika mbili matatizo yao, jambo lililompandisha zaidi hasira Mkurugenzi huyo na kuwaeleza kuwa wanawachochea wenzao kudai haki yao.

"Nawaeleza kabisa kwamba upepo ukivuma ninyi lazima muwepo, ninyi mnachochea wenzenu kuja hapa wizarani. Nimeshawaeleza tatizo lenu linashughulikiwa," alisema kwa ukali.

Karipio hilo lilimfanya mfanyakazi mmoja kumweleza kwa unyonge kuwa wao (wafanyakazi) hawapendi kwenda wizarani na kwamba wanadai haki yao yaani mishahara ya miezi miwili mfululizo.

Kabla mfanyakazi huyo hajamaliza kujieleza, Mkurugenzi huyo alimkaripia: "Nimekwambiaje? Nimesema hivi, hilo jambo limekwishashughulikiwa na hivi sasa vocha za malipo zimeandikwa hadi Ijumaa cheque (hundi) zitakuwa tayari."

Mfanyakazi mwingine alimuuliza iwapo fedha hizo zitakuwa za malipo ya miezi miwili au la ambapo alijibu kwamba ni za malipo ya mwezi Septemba na kwamba mishahara ya Oktoba itashughulikiwa baadaye.

"Uhamisho wetu umekuwa mateso makubwa kwetu. Hivi unavyotuona hapa wengine tunadai sh. 70,000 tu wengine sh. 40,000, sidhani kama kuna mtu anadai sh. 300,000 hapa lakini tunasumbuliwa kiasi hiki," alilalamika mfanyakazi mmoja ambaye ametokea Tanga.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA