TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Sunday, November 15, 2009

Kigogo BoT kukabidhi ofisi chini ya ulinzi

10:39 AM

Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imekubali ombi la Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kumruhusu aliyekuwa Mkurugenzi wa Huduma za benki hiyo, Simon Jengo, kukabidhi ofisi yake chini ya ulinzi wa Mahakama.

Jengo, anakabiliwa na mashitaka ya uhujumu uchumi kwa kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 104. Ombi la kutaka mshtakiwa huyo aruhusiwe kukabidhi ofisi hiyo Novemba 16 na 17, mwaka huu, lilitolewa na BoT katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam jana mbele ya Hakimu Mfawidhi, Joyce Minde.

Mshtakiwa huyo anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na ilifikishwa mahakamani hapo jana kwa kutajwa. Pamoja na Jengo, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Naibu Mkurugenzi wa Fedha, Kisima Thobias Mkango, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Bosco Kimela na Ali Farijalah Bakari, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Huduma za Benki ambao wote ni wafanyakazi wa BoT.

Ombi hilo la BoT lilikubaliwa na Mahakama na kesi hiyo iliahirishwa hadi Novemba 27, mwaka huu itakapotajwa mahakamani hapo.

Hata hivyo, kabla ya kuahirishwa kwa kesi hiyo upande wa mashitaka uliieleza Mahakama kuwa jalada halisi la kesi hiyo bado lipo kwa Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP).

Hivi karibuni, vigogo hao kupitia kwa mawakili wao wanaowatetea walifungua maombi katika Mahakama Kuu wakipinga hoja za upande wa mashitaka (serikali) kutaka wapewe dhamana kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 36 (5), (6) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi ya mwaka 2002 na badala yake waliiomba Mahakama iwape dhamana bila kuzingatia masharti ya kifungu hicho.

Kwa mujibu wa kifungu hicho, washtakiwa hao wanapaswa kutoa kiasi cha Sh.13,019,817 kila mmoja kama dhamana ambazo jumla yake kwa washtakiwa wote wanne itakuwa ni Sh. 52,479268, kiasi ambacho ni sawa na nusu ya hasara wanayodaiwa kuisababishia ya Sh.104,158,636,146.

Mengine ni kusaini bondi yenye thamani ya kiasi hicho zaidi ya Sh. 13 bilioni kila mmoja, kuwa na wadhamini wawili ambao pia watasaini bondi ya kiasi hicho cha fedha, kusalimisha mahakamani hati zao za kusafiria , kuripoti kwa Mkuu wa Upelelezi wa Polisi kila Jumatatu na kutotoka nje ya Dar es Salaam bila idhini ya Mahakama. Wote wameshindwa kutekeleza masharti ya dhamana na wanaendelea kusota rumande.

Wanashtakiwa kwa tuhuma za kuhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh. bilioni 104, wakidaiwa kufanya njama, uzembe au kutochukua hatua kuzuia hasara hiyo kutokea.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA