TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Thursday, November 12, 2009

Augustine Mrema adaiwa kuhusika kuua kilimo kahawa Kilimanjaro

11:15 PM
Na Leon Bahati

CHAMA Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Kilimanjaro (KNCU), kimemtuhumu Mwenyekiti wa TLP,Augustine Mrema, kuwa moja ya sababu za kupotea kwa mwelekea wa kilimo cha zao la kahawa, ambalo sasa uzalishaji wake umeshuka hadi kufikia asilimia 14 ikilinganishwa na miaka ya 1980.

Hata hivyo, Mrema amezikana tuhuma hizo na kurejesha lawama kwa KNCU kuwa ilikuwa inawapora wakulima na alipoidhibiti, ikazembea kufanya kazi zake ipasavyo.

Afisa Uhusiano wa KNCU, Kisuma Mapunda, aliliambia Mwananchi hivi karibuni alipokuwa Naibu Waziri Mkuu katika serikali ya awamu ya pili, Mrema aliiamuru KNCU kuacha mpango wa kuwakata wakulima fedha kwa ajili ya kununua dawa za kuulia wadudu wanaoharibu zao la kawaha.

"Matokeo yake baadhi ya wakulima walishindwa kununua madawa kwenye maduka ya kilimo kutokana na bei kubwa. Vile vile lilijitokeza suala la baadhi ya wafanyabiashara kuwauzia wakulima madawa feki na walipoyatumia hayakuua wadudu na badala yake, yalisababisha mikahawa kufa," alisema Mapunda.

Mapunda alilielezea suala la madawa kuwa ni miongoni mwa sababu saba za msingi, zilizolifanya zao la kahawa mkoani Kilimanjaro kushuka kutoka mauzo ya kilo 21 milioni mwaka 1984/85 hadi kufikia kilo milioni tatu mwaka 2008/09.

Alizitaja sababu nyingine kuwa ni kushuka kwa bei ya zao hilo katika soko la dunia, mikahawa mingi kuzeeka, eneo la uzalishaji kupungua na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yamesababisha joto kupanda huku ikisababisha vipindi virefu vya ukame.

Akijibu shutuma hizo, Mrema alisema hakuizuia KNCU kusambaza dawa kwa wakulima bali aliibana ili isiendelee kuwanyonya wakulima.

"Hawa walikuwa kama waporaji wa wakulima. Walikuwa wanawakata fedha huku wakishindwa kuwasambazia madawa. Nikawa ninawabana wakakosa njia za ulaji, wenyewe wakashindwa kazi," alisema Mrema.

Mrema alisema maelezo ya KNCU ni njama za kutaka kumharibia kisiasa hasa baada ya kutangaza mpango wa kugombea Ubunge katika Jimbo la Vunjo na kujigamba kwamba hawamwezi.



0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA