TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Friday, October 16, 2009

Sumatra yakwama tena kujaribu mabehewa 23

9:07 PM

Jaribio la Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) la kutaka kuyafanyia majaribio mabehewa 23 ya kampuni ya Rites, limekwama kwa mara nyingine tena jana baada ya wafanyakazi kukataa kutekeleza zoezi hilo.

Maofisa wa Sumatra walifika katika stesheni ya Dar es Salaam majira ya saa 1:00 asubuhi wakiwa na polisi kadhaa kwa nia ya kuwashinikiza wafanyakazi wakubali kuyafanyia majaribio mabehewa hayo.

Hata hivyo, Kamanda wa Kikosi cha Reli, aliwazuia askari hao kuingia ndani ya stesheni kuwa hakukuwa na vurugu.

Baada ya maofisa wa Sumatra ambao waliambatana na mkaguzi wao, Eliona Shimbo, kuingia yalipokuwa mabehewa hayo, wafanyakazi walianza kuwazomea huku wakihoji nia ya mamlaka hiyo kuyafanyia majaribio mabehewa ambayo hayajatengenezwa.

"Mliyasimisha haya mabehewa baada ya kubaini yalikuwa na kasoro sasa leo mnayafanyia majaribio bila kuyafanyia matengenezo mnamaana gani?” alihoji mfanyakazi mmoja ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini.

Akizungumza jana, Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi wa Reli (Trawu), tawi la Dar es Salaam, Juma Lema, alisema msimamo wa wafanyakazi hautabadilika kwa kuwa wanania njema ya kuinusuru reli.

Ofisa Uhusiano wa Sumatra, David Mziray, alipohojiwa juu ya hatma ya jaribio hilo alijibu kwa ufupi kuwa 'no comments' (sina la kusema).

Kwa upande wake, Ofisa Uhusiano wa TRL, Midladjy Maez, alisema kampuni yake haihusiki kabisa na zoezi hilo.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA