TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Saturday, October 10, 2009

Serikali kutoa tamko rasmi

2:32 PM

Serikali inatarajia kutoa tamko rasmi kuhusu ongezeko la gharama za huduma kwa wagonjwa wa Rufaa Binafsi (Private Patients) zilizopandishwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuanzia Oktoba Mosi mwaka huu.

Hatua hiyo ya wizara kujipanga kutoa tamko imekuja ikiwa imepita siku moja baada ya wananchi wanaotumia huduma hiyo hospitalini hapo kutoa malalamiko kwa serikali kuwa ongezeko hilo halikulenga kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini wanaohitaji huduma hiyo.

Akizungumza jana na Nipashe, Afisa Uhusiano wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Sanchris Mwamwaja, alisema kutokana na kupokea malalamiko ya wananchi kwa njia ya magazeti, wizara imeamua kutoa tamko lake rasmi juu ya ongezeko hilo.

Mwamwaja alisema kwa sasa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Blandina Nyoni, anaandaa maelezo ambayo ndiyo yatakuwa tamko la wizara.

"Muda wowote wizara itatoa tamko kuhusiana na upandishwaji wa gharama za huduma ya rufaa binafsi iliyopandishwa hospitali ya Muhimbili, siwezi kusema itatolewa lini lakini tupo katika hatua nzuri ya utoaji wa tamko hilo," alisema

Aidha, alisema wananchi wanatakiwa kuwa na subira wakati wizara ikishughulikia malalamiko na manung'uniko ya wananchi juu ya gharama hizo.

Baada ya hospitali ya Muhimbili kupandisha huduma hiyo mwezi huu kwa maelezo kuwa ni katika kuongeza kipato cha hospitali ili iweze kutoa huduma bora zaidi, baadhi ya wananchi walilalamikia hatua hiyo na kusema kuwa haijazingatia hali halisi ya Watanzania kimapato.

Aidha, wananchi walisema kitendo cha hospitali ya serikali kuongeza gharama hizo hakijazingatia hali ya uchumi wa wananchi walio wengi ambao ni maskini.

Baadhi ya huduma ambazo gharama zake zimepandishwa hospitalini hapo ni maabara, meno, damu, picha ya mionzi, mawimbi ya sauti na picha ya kutumia sumaku.

Gharama nyingine zilizopanda ni kulazwa, kuona daktari na upasuaji. Gharama za upasuaji zimepanda hadi kufikia zaidi ya Sh. milioni moja.

Wakati huo huo, Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu, amemtaka Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa, kuangalia upya gharama za vipimo Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Akizungumzia kupandisha gharama za vipimo jana, Zungu alisema aliwahi kumtahadharisha Profesa Mwakyusa hali ya gharama za matibabu kwa hospitali za serikali.

Alisema alitarajia kupata majibu ya suala hilo, lakini kinyume chake gharama zimepanda maradufu bila kuzingatia hali ya mtu wa chini.

Zungu alisema hospitali za serikali zinapata ruzuku ambayo inachangia kupunguza hali ya kuwabebesha mzigo wa gharama za uendeshaji wagonjwa, na kwamba zoezi lolote la kupandisha bei lazima lizingatie uwezo wa mwananchi wa kawaida, ikiwa ni pamoja na mfanyakazi wa kima cha chini serikalini.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA