TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Sunday, October 11, 2009

Bilioni 2.9/- kugharamia usambazaji maji Kilimanjaro

10:24 AM
Wizara ya Maji na Umwagiliaji imetoa zaidi ya sh. bilioni 2.9 kwa ajili ya utekelezaji wa programu ya usambazaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa maeneo ya vijijini mkoani Kilimanjaro ili waweze kuondokana na kero ya maji.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya, aliyasema hayo jana wakati akiongea na wafanyakazi wa Mamlaka ya majisafi na majitaka mjini Moshi (Muwsa) katika ziara yake ya siku mbili mkoani Kilimanjaro.

Alisema serikali kupitia wizara yake na wafadhili mbali mbali wamekuwa wakitekeleza azma ya kuwapatia maji safi na salama wananchi wa vijijini ili kuondokana na adha ya upatikanaji wa maji na kuondokana na umasikini.

Mwandosya alitoa wito kwa mamlaka hiyo kuanzisha ushirikiano wa kutunza vyanzo vya maji na misitu iliyopo katika hifadhi ya mlima Kilimanjaro na kuwa na vyanzo endelevu vya maji ambapo pia aliagiza mamlaka hiyo kusimamia kikamilifu kazi zinazofanywa na wahandisi wa maji kwa kufuatilia taarifa za utekelezaji wa programu ya maji vijijini.

Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi, Antony Kassonta, alisema mamlaka yake imepokea Sh. 925,552,124 kwa ajili ya utekelezaji wa programu ya maendeleo ya usambazaji wa maji katika wilaya za Mwanga, Same na Himo Wilaya ya Moshi vijijini.

Alisema programu ya maendeleo ya sekta ya maji katika mji wa Same utahusisha vijiji 37 katika wilaya za Mwanga, Same na Korogwe na kwamba mradi huo utahusisha utoaji wa maji kutoka bwawa la Nyumba ya Mungu.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA