TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Wednesday, October 28, 2009

12:55 AM

Rais Jakaya Kikwete amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Mfalme Mohammed wa Morocco, ulioletwa na mshauri maalum wa Mfalme, Yassine Mansouri.

Katika ujumbe huo, Mfalme Mohammed alisema amekubali mwaliko kutoka kwa Rais Kikwete kutembelea Tanzania uliotumwa kwake na kusisitiza nia ya nchi hizi kufufua na kukuza uhusiano baina yao.

Naye Rais Kikwete alielezea nia na dhamira ya dhati ya serikali yake kufufua uhusiano wa nchi hizi ili kukuza biashara na diplomasia.

Mansouri alitumia fursa hiyo kumweleza Rais Kikwete masuala mbalimbali ya kisiasa na kiuchumi.

Wakati huo huo, Rais aliondoka jana jioni kuelekea mkoani Iringa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu baadaye ataelekea Mbeya kwa ziara nyingine ya kikazi ya muda kama huo.

Akiwa Iringa na Mbeya, Rais atakagua na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na wananchi kabla ya kurejea Dar es Salaam.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA