TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Wednesday, October 28, 2009

10:27 PM

Kesi dhidi ya Liyumba kuendelea mwezi ujao


Kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 200, inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Armatus Liyumba, itaendelea kusikilizwa kuanzia Novemba 18 hadi 26 mwaka huu.

Kesi hiyo inasikilizwa na mahakimu watatu ambao ni Edson Kasimwongo, Lameck Mlacha na Benedict Mwinga katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Hata hivyo, kesi hiyo itakuja tena Novemba 11 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa kabla ya kuanza kusikilizwa kwa siku nane mfululizo.

Upande wa mashtaka unatarajiwa kuleta mashahidi kumi, ambapo mashahidi wawili wameshatoa ushahidi wao.

Katika shauri hilo, Liyumba anatuhumiwa kutumia madaraka yake vibaya na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 221, kupitia kwenye mradi wa ujenzi wa majengo pacha ya benki hiyo

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA