TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Wednesday, October 14, 2009

Majeruhi wa risasi wapata ahueni Nigeria

7:40 PM

Nigeria imeondoa sheria iliyolazimisha hospitali kutotoa huduma za dharura kwa watu wanaoshambuliwa kwa kupigwa risasi mpaka kupokea ripoti ya polisi.

Maafisa walibatilisha sheria hiyo iliyokuwepo tangu miaka ya 80 kutokana na kuwepo kwa ongezeko la watu waliofariki dunia kwa majeraha ya risasi.

Sheria hiyo imeondoshwa baada ya mhariri wa gazeti moja, Bayo Ohu alipofariki dunia kutokana na majeraha ya risasi baada ya hospitali kusubiri ripoti ya polisi badala ya kumtibu.

Nigeria ina matukio mengi ya uhalifu unaohusu matumizi ya bunduki ikiwemo utekaji nyara na ujambazi.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA