TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Friday, October 2, 2009

Majambazi yala bao

10:45 AM

Watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamepigwa bao baada ya wananchi kuwazuia kufanikisha uporaji wa gari ambalo waliliiba pale kwenye maduka ya Shoppers Plaza yaliyopo Mikocheni, Jijini Dar es Salaam.

Imedaiwa kuwa baada ya watu kupora gari hilo walijaribu kuondoka nalo, lakini kabla hawajafika mbali, likawatupa mtaroni.

Mmoja wa askari wanaolinda maduka hayo, alisema yeye na walinzi wenzake wakiwa eneo hilo waligundua kuwepo kwa watu watatu waliowahisi kwamba ni wahalifu.

Akasema waliwaendea watu hao na walipojaribu kuwahoji wakadai kuwa wanamsubiri mtu aliyeingia ndani ya duka.

Akasema hata hivyo baada ya muda waliwaona tena watu hao wakiingia ndani ya gari dogo aina ya saloon na kisha kuondoka nalo kwa kasi, hali iliyowatia mashaka na kuamua kupiga filimbi za kuashiria hatari.

Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema waliona gari hilo likiendeshwa kwa kasi kubwa huku watu wakiliitia mwizi! mwizi ! na ndipo walipojaribu kulitupia mawe na wengine kujipanga barabarani.

Kwa mujibu wa mashuhuda hao, wakati majambazi hayo yakijaribu kuwakwepa ndipo gari hilo lilipoingia mtaroni na majambazi hao watatu kutimkia kusikojulikana.

Ofisa Mtendaji wa kata hiyo, Bw. Silivester Mtonja, amesema kumeibuka vitendo vingi vya uporaji katika maduka ya eneo hilo na kwamba wezi wamekuwa wakikimbilia katika mitaa iliyopo ndani ya kata yake.

Amesema wezi hao wamekuwa wakipora pochi za wanawake kisha kukimbilia katika maeneo hayo, jambo ambalo limekuwa likihatarisha maisha ya wakazi wake.

Amewaomba Polisi kuongeza ulinzi katika eneo hilo ili kukomesha vitendo hivyo ambavyo vimeshika kasi.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa majambazi hayo hayakufanikiwa kuiba kitu chochote baada ya wananchi kuzima jaribio hilo.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA