TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Monday, October 26, 2009

Hivi ndivyo Lowassa alishiriki Richmond

3:19 PM

Kilio cha Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa (pichani), bungeni kwamba alidhalilishwa sana kwa kuhusishwa na mkataba tata wa kampuni ya Richmond, si lolote wala chochote baada ya uchunguzi wa kina wa nyaraka uliofanywa na gazeti hili kubaini kwamba alihusika vilivyo katika mchakato mzima wa zabuni hiyo.

Nyaraka kadhaa ambazo Nipashe imeziona, zimethibitisha si tu ushiriki wa Lowassa katika mchakato huo, bali alikuwa anatoa maelekezo ya nini kifanyike kwa kila hatua.

Nyaraka hizo zinaonyesha kwamba Waziri wa Nishati na Madini wakati huo, Dk. Ibrahim Msabaha, alibakia kuwa kama karani tu wa kutekeleza maagizo ya Lowassa, kila hatua alikuwa anaamua Lowassa na kuifanya Wizara ya Nishati na Madini kutekeleza kile alichotaka kiongozi huyo aliyejiuzulu Februari mwaka jana huku akilalamika kwamba ameonewa kwa kuzushiwa mambo kuhusu kashfa ya Richmond. soma zaid


1 comments:

chib said...

Heeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!

Post a Comment

 
BONYA HAPA