kwa heshima na upendo ninapenda kupitia mtandao huu wa jamii kuwajulisha watanzania wenzangu juu ya ugeni katika jiji la Dallas Texas. Mchungaji MALAS (Pichani) pamoja na mke wake kutoka Tanzania wapo katika jiji letu.
Kwa wasio mfahamu, Mchungaji Malasi ndiye muanzilishi wa huduma ya MKESHA MKUBWA WA MAOMBI KATIKA NCHI YETU YA TANZANIA.Mungu alimpa huyu mtumishi maono ya kuwaunganisha watu wote bila kujali dini zao na kuomba kwa pamoja katika mkesha wa kufunga mwaka.Kupitia huduma hii maelfu kwa maelfu ya watu wamekuwa wakikusanyika katika Uwanja wa Taifa pale DSM na kuomba kwa pamoja.
Kwa heshima na upendo ninapenda kumkaribisha kila mtu katika jiji hili la Dallas na vitongoji vyake katika semina itakayoanza siku ya Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kuanzia saa 12 jioni katika kanisa la Umoja.
Kwa wale walio mbali na wanajamaa katika jiji hili tunaomba muwajulishe.
Anuani;
Umoja Church
Hillcrest Rd
Dallas Texas,
75230
Simu;Pastor Absalom Nasuwa; 214 554 7381

0 comments:
Post a Comment