TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Friday, September 4, 2009

Waziri wa JK asusiwa mkutano

9:21 PM

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Adam Malima, amejikuta katika wakati mgumu wa kujibu vyema kero za baadhi ya wananchi wa jimbo lake la Mkuranga baada ya kususiwa mkutano na wajumbe kibao wa Serikali ya Kijiji alichotembelea.

Naibu Waziri huyo, ambaye pia ni Mbunge wa Mkuranga, amekutwa na masahibu hayo hivi karibuni wakati akiwa katika Kijiji cha Kimanzichana, ambako alikuwa akifanya mkutano uliokuwa sehemu ya majukumu aliyokuwa nayo katika kufanikisha ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali jimboni humo.

Baada ya kujikuta akitoswa na wajumbe wengi ambao hawakuhudhuria mkutano wake huo, Malima akaeleza wazi kuwa amekerwa na hasa kwa vile uongozi wa kijiji hicho (cha Kimanzichana) wameshindwa kusimamia vyema shughuli za maendeleo.

Serikali hiyo ya Kijiji cha Kimanzichana, inaundwa na wajumbe 20, ambapo kati yao, 18 wanatokea Chama cha Wananchi, CUF na wawili pekee ndio wa Chama Cha Mapinduzi, CCM.

Malima akasema kijiji hicho kina wakazi zaidi ya 17,000, lakini kutokana na uongozi uliopo, wakazi wake wameshindwa kuhamasisha wananchi ili wajitolee katika ujenzi wa Sekondari ya Kata na pia Zahanati ya kijiji.

Akadai kuwa kilichomkera zaidi, ni wajumbe hao kutokuhudhuria mkutano wake huo alioamua kuufanyia kijijini hapo kwa lengo la kutaka kujua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wake.

Amesema baadhi ya majibu ya kero zilizopo yangepatikana toka kwa viongozi wa Serikali ya Kijiji ambao wengi wamekacha na badala yake kuwepo wawili tu ambao ni wa kutoka CCM.

Katika ziara hiyo ya siku kumi, Malima aliahidi kutoa shilingi milioni moja kwa ajili ya ujenzi wa Sekondari ya Kata ya Mwalusembe, katika Kijiji cha Bigwa.

Pia akawahimiza wananchi juu ya kilimo cha michikichi, mihogo na maembe ya kisasa.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA