
Tumaini Msowoya na Thomas Ludovick.
ZAIDI ya watoto 175, wamezaliwa katika mkesha wa sikukuu ya Idd el fitri, jijini Dar es Salaam.
Watoto 101 kati ya hao walizaliwa katika hospitali ya Wilaya ya Temeke,wengine 56 katika hospitali ya Ilala wakati watoto 18 walizaliwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakunga wauguzi wa hospitali za Wilaya ya Temeke, Ilala na Hopitali ya Taifa ya Muhimbili walisema watoto 89 kati ya wote waliozaliwa ni wa kike wakati watoto 86 ni wa kiume 86.
Mkunga muuguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Mary Mwakyusa alisema watoto 18 waliozaliwa hapo, wazazi walijifungua kwa njia ya kawaida na kwamba hali zao zinaendelea vizuri.
"Tunashukuru Mungu wazazi wote wamejifungua salama, wengi wao wameruhusiwa na wengine waliobaki wanaendelea na matibabu licha ya kuwa afya zao zimetengemaa," alisema Mwakyusa.
Kwa upande wa Temeke, Afisa Muuguzi wa hospitali hiyo, Alphonce Chimwambo alisema kuwa watoto 48 walizaliwa Idd mosi wakati wengine 53 walizaliwa Idd pili na kuwa hakuna aliyejifungua kwa njia ya upasuaji,
"Wote wamejifungua salama na tayari wameruhusiwa kwa sababu hakukuwa na upasuaji wowote,"alisema
Mzazi mmoja wa katika hospitali hiyo, Eva Mlagala Mkazi wa Gongolamboto alisema alifurahi kumpata mtoto wa kiume hasa wakati wa sherehe hizo.
"Namshukuru Mungu kwa kunipa mtoto wa kiume akiwa hai. Wengine wawili niliowahi kujifungua walifariki. Nimefurahi sana", alisema Mlagala
0 comments:
Post a Comment