Mradi wa kufukia bahari wakwama Dar es Salaam
MRADI wa kubadilisha mandhari ya ufukwe wa Bahari ya Hindi maarufu kama Salama Water Front, umekwama baada ya kampuni iliyokuwa imeomba kuutekeleza kushindwa.
Serikali imeamua kuipa notisi kampuni hiyo ya Coastal Developers Co-operation yenye kushirikisha wanahisa kutoka Afrika Kusini, Uholanzi na Tanzania.
Serikali imeamuru zabuni hiyo itangazwe kwa wawekezaji wengine.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Emmanuel ole Naiko, awali kampuni hiyo iliipa matumaini Serikali, kwamba ingeweza kutekeleza mradi huo haraka.
Baada ya kuonekana hakuna utekelezaji unaofanyika, Kamati ya Waziri Mkuu ilikaa mwaka juzi kwa ajili ya suala hilo.
Kupitia kamati hiyo, kampuni ilipewa mwaka mmoja wa kujipanga zaidi lakini hakuna kilichofanyika.
Naiko amesema,mwaka huu, wenye kampuni hiyo waliitwa na wakatoa sababu kwamba wanajaribu kukamilisha masuala ya kifedha, jambo ambalo hata hivyo, Serikali haikuridhika nalo.
Home
»
»Unlabelled
»
7:58 PM
Mshirikishe Mwezako Kupitia:
0 comments:
Post a Comment