TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Sunday, September 13, 2009

11:52 PM
washiriki wa filamu kali ya 'baby powder'' wavamia washington DC
Mcheza filam ya Bbay Powder na rapper Justellh akiwa na Sunday Simba Shomary, mtangazaji wa VOA idhaa ya kiswahili katika mnuso wa Labour Day weekend Washington DC ikiwa ni katika pilika pilika za kutangaza filam hii mashuhuri itakayoanza kuonyeshwa kwa mara ya kwanza huko Atlanta Georgia mwezi Novemba mwaka huu.
Fundi Ima akiwa amezungukwa na wacheza filam wa Baby Powder kushoto kwake Justellh na kulia kwake Tuni na Wada ambao ni mashoga katika filamu ya Baby Powder.

Hawa ni baadhi ya wasanii waliocheza filamu ya Baby Powder walipovamia jiji la Washington Dc katika kutangaza filam yao na kusheherekea Labour Day weekend. Kutoka kushoto Sajo,Babu Sikari-rapper na mcheza filam,Tuni muigizaji mwandamizi wa kike,Lambert a.k.a LBT muigizaji mkuu na Justellh muigizaji na rapper machachari wa ATL.

Kundi la baadhi Waigizaji wa Baby Powder na maprodyuza wao.
Picha zote kwa hisani ya Sunday Shomary


MWANDANI WA BABY POWDER
PHILIP NKASA (Lambert "LBT" Tibaigana) ni kijana wa kitanzani anakwenda marekani kwa matumaini ya kupata elimu ili kuweza kuboresha maisha yake na ya familia yake nyumbani. Philip ananzaa maisha yake ndani ya marekani katika mji mdogo wa Wichita,KS na baada ya kumaliza shule na kushindwa kupata kazi ,Philip anakata shauri kwenda kujaribu bahati yake katika jiji la Atlanta, GA.
Mambo hayawi kama Philip alivyo tegemea upatikanaji wa kazi Atlanta unakua wa shida,ili kuendesha maisha Philip anachukua kazi ya malipo kidogo pamoja na kuaa ana degree...hali ya maisha ya wazee wake inaendela kua mbaya kutokana na mapato yake kidogo anashindwa kuwasaidia,Baada ya kugundua mfanyakazi mwenzake Mamdo (Albert Levasseur) anafanya biashara haramu, Philip anona nafasi ya kutatua matatizo yake...

Lakini baada ya kuonja asali anachonga mzinga na kuingia katika biashara haramu kwa nguvu zote. kutokana na kukua kwa biashara yake Philip anaoneza msaada kutoka kwa vijana wenzake Tizo ( Carlos Mwaibulla) Chuma (Ulimboka GWAII Mwanjabala) Wesi (Hadji saidia) kwenye wengi hapa haribiki jambo lakini kundi hili linaubadilisha msemo huo....( mengi yana haribika)Philip anaingia mapenzi na mrembo kuoka Kenya WARIDI (Tuni Ngigi) ambaye anashindwa kumuambia ukweli kuhusu biashara zake,lakini za mwizi arobaini,Waridi anakuja kugundua...utamu unafikia kilele hapo.....
Majina ya waigizaji
Lambert Tibaigana- PHILIP NKASA
Tuni Ngigi WARIDI
Carlos Mwaibulla TIZO
Ulimboka Mwanjabala CHUMA
Hadji Saidea WESI
Lydia Mbuah JOSELYNE
Warda Hassan JACKEY
Dynamic DULAH
Albert Levasser MAMADO
Babu sikare KAI
na wengine wengi....

BABY POWDER ni filamu inayo elimisha, sikitisha ,furahisha,na kutia moyo...na ni mkasa wa kuburudisha...Filamu hii haita toka kwenye DVD mpaka mkatikati ya mwaka 2010 nafasi pekee ya kuiona filamu hii ni wakati wa uzinduzi rasimi katika sehemu mbali mbal.

Kwanza kabisa BABY POWDER itazinduliwa rasmi:
*ATLANTA,GA November 14th 2009,
*HOUSTON,TX ( November 26th 2009)
*WASHINGTON DC ( December 5th 2009)
*MINNESOTA ( December 19th 2009)
tour ya AFRICA/EUROPE kuanzia DECEMBER 25th 2009

tembelea
www.jake-productions.com
au angalia

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA