TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Friday, September 4, 2009

Wagombea wa CCM wachoma moto karatasi za kupigia kura

1:31 PM

Baadhi ya wagombea wa uenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa vitongoji na vijiji vya Wilaya za Tarime na Rorya mkoani Mara na wapambe wao, wamefanya vurugu na kuchoma karatasi za kupigia kura kwa madai kuwa zimezidi idadi ya wanachama wa matawi ya maeneo yao.

Katibu wa CCM wa Wilaya hizo, Livingstone Lusinde jana alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo na kuchomwa moto kwa karatasi kulikofanywa na wapambe wa wagombea.

Lusinde alisema wagombea hao ni miongoni mwa wa vijiji 78 na vitongoji 376 wakiwamo wanaotetea nafasi hiyo waliojitokeza katika kinyang'anyiro hicho ndani ya CCM.

Kwa mujibu wa Lusinde, wanachama wa CCM katika vijiji 50 kati ya hivyo na vitongoji 210 ndiyo waliopiga kura katika uchaguzi huo ulioanza kufanyika hivi karibuni.

Lusinde alivitaja vijiji ambako vurugu hizo zilitokea kuwa ni Nkende, ambako mwenyekiti anayetetea kiti hicho, John Maburugi alibwagwa na Faustine Marwa kwa kura 159 baada ya kuambulia 104.

Alisema baada ya matokea hayo kutangazwa, wapambe wa mgombea huyo wanadaiwa kufanya vurugu na kuchoma karatasi za kupigia kura wakidai wanachama waliongezeka kuliko idadi kamili ya wanachama wa tawi la kijiji hicho.

Vile vile, alisema Makamu Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Tarime alianguka katika Kitongoji cha Buhemba kwa kupata kura 60.

Katika kitongoji hicho, mpinzani wake aliyetajwa kwa jina moja la Ibrahim, alishinda kwa kupata kura 61.

Naye Mwenyekiti wa Mamlaka hiyo, Mwita Mantago, alitetea kiti chake kwa kuzoa kura 42 dhidi ya Yusuf Sarungi aliyeambulia kura tano tu.

Vijiji na Vitongoji vingine vilivyokumbwa na vurugu za kuchomwa moto kura ni pamoja na Vijiji vya Nyakunguru, Bukwe, na Nyanungu.

Katika maeneo hayo ilidaiwa baadhi ya wenyeviti wa zamani walikuwa wakiuza kadi ili kuongeza idadi ya wapiga kura na kusababisha vurugu hizo.

Lusinde alisema majina sita kati ya nane ya wagombea walioomba kugombea uenyekiti wa katika baadhi ya vitongoji na vijiji yarirudishwa.

Uchaguzi wa wenyeviti wa wilaya za Tarime na Rorya utafanyika baada ya kupata baraka kutoka Mkutano wa Halmashauri ya Mkoa wa Mara.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA