TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Tuesday, September 29, 2009

1:27 PM

Waathirika Mbagala `wavamia` ofisi ya Pinda


Waathirika wa milipuko ya mabomu Mbagala, wamevamia ofisi ya Waziri Mkuu, jijini Dar es Salaam, wakitaka kujua kuhusu hatma ya malipo ya fidia zao.

Pia wamesema kuendelea kuishi kwenye mahema huku kukiwepo taarifa za tishio la mvua za El-Nino, ni hatari kwa maisha yao.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya kundi la waathirika hao kutumia mbinu ya kuvikwepa vyombo vya ulinzi na usalama kwa kila mtu kuondoka kivyake na kukutana katika ofisi hizo saa 3:00 asubuhi jana.

Hata hivyo, jaribio la waathirika hao la kutaka kumuona Waziri Mkuu jana, liligonga ukuta, baada ya kuzuiwa na maofisa usalama waliopo kwenye mapokezi ya ofisi hizo.

Maofisa hao waliwazuia na kuwataka kufuata taratibu za kuwasilisha madai yao kwa Waziri Mkuu, badala ya njia waliyotumia jana.

Mmoja wa waathirika hao, Devotha Benjamin aliliambia Nipashe jana kuwa wamelazimika kuvamia ofisi hizo ili kupata ufafanuzi kutoka kwa Waziri Mkuu kuhusu hatma ya malipo ya fidia zao.

Alisema sababu nyingine, inahusu kundelea kwao kuishi kwenye mahema, hasa katika kipindi hiki ambacho kuna tishio la kunyesha mvua za El-Nino nchini.m

Zoezi la ulipaji fidia kwa waathirika wa Mbagala, lilianza Agosti 24, mwaka huu, huku baadhi wakilalamika kulipwa fedha kidogo kulinganisha na thamani halisi ya uharibifu wa nyumba zao na wengine wakikosa kulipwa kabisa.

Mabomu hayo yalilipuka katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) iliyoko Mbagala Kuu, Aprili 29 mwaka huu na kusababisha watu 26 kupoteza maisha, wakiwamo askari sita wa JWTZ, baadhi ya nyumba zilizokuwa jirani na kambi hiyo kubomoka kabisa, nyingine kuharibika kwa viwango tofauti, na pia samani kuharibika.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA