
Ni rasmi sasa, hakuna timu yoyote kutoka Afrika mashariki na kati ambayo itashiriki katika fainali za kombe la dunia mwaka ujao Afrika Kusini, labda kama watazamaji tu wa kuwashangilia magwiji wa soka kutoka Ghana, pengine Ivory Coast na videdea kutoka kaskazini.
Kilichobaki ni majuto na kibarua kigumu cha kujaribu kung'ang'ania fursa ndogo ya kuingia katika fainali za kombe la mataifa ya Africa, Cup of Nations, zitakazofanyika Angola mwezi Januari, mwakani.
Pengo hilo ni dogo na litahitaji timu za Kenya, Rwanda au hata Sudan kupambana kufa na kupona katika mechi zilizosailia ili kuonekana kihalali nchini Angola.
Ukitizama Afrika ya kati, waakilishi Zambia na Malawi wanademadema huku kombe la dunia likibaki ndoto mbaya na safari ya Angola ikiwa imejaa magugu na miiba ya upinzani mkali kutoka magharibi na kaskazini.
0 comments:
Post a Comment