Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) anayeshughulika shirikisho, Beatrice Kiraso, amesema kitendo cha majeshi ya nchi tano wanachama wa jumuiya hiyo kufanya mazoezi ya kijesi kwa pamoja ni ishara ya kuaminiana miongoni mwa nchi wananchana.
‘’Zoezi hili linamaanisha kwamba tumejenga kuamiana vya kutosha na ni ishara kwamba majeshi yetu hayatageukiana kupambana yenyewe kwa yenyewe,’’ Kiraso aliwaambia waandishi wa habari Ijumaa mkoani Arusha na kuongeza kwamba ‘’majeshi yetu sasa yanafanya shughuli kama jeshi moja.’’
Alisema kipindi cha miaka 10 ya uhai wa jumuiya hiyo iliyozinduliwa upya mwaka 1999 baada ya kufa kwa ile ya awali mwaka 1977 kasi ya ushirikiano ilikuwa ndogo kutokana na haja ya kujenga moyo wa kuaminiana miongoni mwa wanachama.
Awali Jumuiya hiyo iliundwa na nchi tatu za Kenya, Uganda na Tanzania lakini kwa miaka ya hivi karibuni Rwanda na Burundi nao walijiunga na kuongeza idadi ya wanachama kufikia nchi tano sasa.
Kwa mujibu wa Kiraso zoezi la pamoja la kijeshi kutoka majeshi ya nchi tano wanachama (CJTF) linalojuilikana kama ‘’Zoezi Mlima Kilimanjaro’’ litafanyika katika mikoa ya Arusha na Tanga kwa majibu wa makubaliano ya ushirikiano katika maswala ya ulinzi miongoni mwa nchi wananchama.
Zoezi hilo litakalogharimu dola za Kimarekani milioni 2.4, sawa na zaidi ya shilingi za Tanzania bilioni 2.4 linalenga kuwapa mfunzo ya pamoja majeshi ya nchi wananchama kuweza kufanya opereheni za pamoja za kulinda amani, kupambana na ugaidi na namna ya kukabiliana na majanga.
Kwa mujibu wa Kiroso zoezi hilo litaimarisha majeshi ya EAC kuwa tayari kukabiliana na matatizo katika hali halisi ya mazingira ya ukanda huu wa Afrika Mashariki.
Zoezi hilo la kwanza la aina yake kuhusisha majeshi ya nchi kavu, anga na majini pamoja na silaha na zana nyingine za kijeshi litahushiha wanajeshi na raia 1,556 toka nchi zate tano wakiwemo wadau muhimu kama vile polisi, uhamiaji, vitengo vya maafa, usalama wa taifa, wizara za mambo za nje, mashirika mbalimbali ya kimataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO).
Pamoja na mambo mengine majeshi hayo katika zoezi hilo pia yatagawa chakula kwa maeneo yanayokabiliwa na njaa na pia watatoa huduma za uchunguzi wa afya za wananchi katika maeneo watakayopitia.
Zoezi hilo ambalo litafunguliwa rasmi na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania Jumapili, Agosti 6, katika Chuo cha Kijeshi cha Monduli mkoani Arusha litahitimishwa Septemba 23, mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment