TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Monday, September 28, 2009

Pinda akataza ununuzi wa magari ya kifahari

8:37 PM
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amewaagiza watendaji wa Serikali watafute namna ya kupunguza matumizi ya fedha za umma ikiwa ni pamoja na kutonunua magari ya kifahari.

Amewataka watendaji hao wabadilike, waache ubinafsi, na wasijifikirie wao tu, kuna mamilioni ya watanzania wanaohitaji fedha kidogo zilizopo.


Waziri Mkuu ametoa mfano kuwa, katika Wizara za Serikali kuna magari mengi ya aina ya Toyota Land Cruiser VX yanayouzwa kati ya Sh milioni 160 hadi 220 na kwamba Tanzania sin chi ya neema kiasi cha kutaka ufahari kiasi hicho.


“Watanzania hembu tubadilike, kuna watu kule chini wanahitaji hizi fedha kidogo tulizonazo” amesema Waziri Mkuu.


Pinda amesema, Serikali isiponunua magari hayo ya kifahari kwa miaka miwili au mitatu maisha ya watanzania yatabadilika kwa kuboresha kilimo na sekta ya mifugo.


Waziri Mkuu amesema, kuna mtazamo usio sahihi miongoni mwa watumishi wa Serikali, viongozi ni wabinafsi, na kwamba, wanajifikiria wao tu.


“Lakini mindset za watanzania bado bado kweli kweli” amesema Waziri Mkuu mjini Dodoma, wakati anafungua mkutano wa siku tatu wa Watendaji wa Serikali na wadau wa sekta ya mifugo.


1 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Pengine Waziri Mkuu angetambua kuwa alishasema haya na mpaka sasa alistahili kuwa ametekeleza. Narejea toleo langu la Februari 11 mwaka huu (http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/02/gari-moja-matrekta-20-uwiano-mzuri.html)ambapo mwenyewe Mhe. Pinda alisema kuwa wamegundua kuwa GARI MOJA LINA THAMANI SAWA YA MATREKTA 20 na kuwa angehakikisha kuwa hakuna nyongeza ya mishahara mwaka huu bali wanaelekeza pesa kwenye mambo muhimu kama magari ya zimamoto na matrekta ili kuinua kilimo nchini. Ni kipi kilichoripotiwa baada ya hapo? Wabunge wameongeza mishahara ya watumishi wa juu wa Serikali na kusahau aliyosema. Sijui ni ugonjwa gani wa kusahau unaowakumba viongozi na sijui kwanini vyombo vyenye kurekodi kauli hizi visiwasute na kuwarejeshea kumbukumbu kuwa "walishahubiri" huu uongo wausemao?
Lakini hii ndio Tanzania yangu, iliyo na vyombo vingi vya habari visivyo na habari zaidi ya taarifa (http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/09/tanzania-yangu-yenye-vyombo-vingi-vya.html)
Tuendelee kuwasikiliza wanavyoanza kubwabwaja kuelekea uchaguzi ujao

Post a Comment

 
BONYA HAPA