Rais Barack Obama , amesema andhamiria kufanya kitu flani kuhusiana na mpango wa mabadiliko ya sekta ya afya, mwaka huu.Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha ABC, ikiwa ni utangulizi wa hotuba yake kwa baraza la Congress, Obama amesema kwamba , yupo wazi kwa ushauri na amesema kuwa hatakuwa mtu asiyebadili msimamo, au mtu anayeng'ang'ania itikadi.
Bwana Obama amesema kuwa "Hotuba yangu itatoa ufafanuzi wa kina juu ya kile ninachokifikiria kuwa , ni njia nzuri ya kwenda mbele ".
Wajumbe wa baraza la Congress wanajiandaa kutaka kujua undani wa sera ya mabadiliko ya sekta ya afya , baada yamapumziko ya kipindi cha kiangazi.
Rais anataraiwa kuzungumzia mgawanyiko wa kisiasa uliojitokeza kufuatia mpango wa kuwa na mfuko wa bima wa uma.
Alipoulizwa kuwa Je? wamarekani watajua baada ya hotuba yake kuwa atasaini au hatasaini , muswada wa mabadiliko ya sekta afya bila kujumuisha swala la mpango wa bima ya uma.
Amesema "Nadhani umma utajua, ni nini nafikiria kitatua mataizo ya mfumo wetu wa afya". Obama amesema kuwa hotuba yake itaelekezwa kwa wananchi , vilevile kwa wajumbe wa baraza la Congress.
Malengo ya hotuba hii ni ,'A', kuufanya umma wa wamarekani kufahamu ni nini tunapendekeza, aesema Bwana Obama.
Na, 'B', kuwafanya wana Democrats na Republican kufahamu kuwa nipo wazi kwa ushauri, na sitakuwa mtu asyekubali mabadiliko na anayeng'ang'ania itikadi katika swala hili. Lakini tunadhamiria kufanya kitu flani mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment