TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Thursday, September 3, 2009

Mnigeria akiri mafunzo Afghanistan

11:07 PM

Mwanachama wa dhehebu la kiislam la Nigerial lililohusika na vurugu za hivi karibuni nchini humo amekiri kupokea mafunzo nchini Afghanistan, polisi wanasema.

Mwanachama huyo wa wa dhehebu linalofahamika nchini humo kama Boko Haram na Taliban amesema alilipwa dola 500 za kimarekani kuhudhuria mafunzo hayo na aliahidiwa kulipwa dola 35,000 za kimarekani amalizapo.

Kuibuka kwa kundi hilo kumesababisha watu 700 kufa wengi wao wakiwa ni wapiganaji.

Iwapo itathibitishwa itakuwa ni ushahidi wa kwanza kuhusishwa kwa waislamu hao katika nchi tajiri ya mafuta na Afghanistan.

Watu wa Nigeria wanaliita kundi hilo Taliban kwasababu imani yao ya msimamo mkali.

Kwa miaka kadhaa wanadiplomasia wamekuwa wakihofia kuwa al-Qaeda huenda wakaazisha mashambulio katika miundo mbinu ya mafuta nchini Nigeria ambayo imekuwa ni msambazaji kubwa wa mafuta kwa Marekani.

Mtu huyo mwenye umri wa miaka 23 Abdulrasheed Abubakar, aliletwa kwa waandishi wa habari katika jimbo la Borno makao makuu Maiduguri, kulikokuwa mako ya kundi hilo, na kushuhudia vurugu mbaya sana.

Polisi pia walionyesha kiasi kikubwa cha silaha na kifaa cha kutengenezea mabomu vilivyokamatwa kutoka kwa watuhumiwa wa kundi hilo la Boko Haram waliokamatwa hivi karibuni katika miji ya kaskazini ya Yola na Maiduguri.

Bilkisu Babangida wa BBC anasema Bwana Abubakar alionekana mwenye ujasiri asiye na wasiwasi kabisa mbele ya waandishi wa habari.

Alielezea kuwa aliingia katika uislam miezi saba iliyopita na kuamua kujiunga na kundi hilo baada ya kununua mafundisho ya kiongozi wa Boko Haram Mohammed Yusuf katika mkanda wa kaseti.

''Ilikuwa ni hisia za mafundisho ya Mohammed Yusuf - nguvu iliyoniwezesha kujiunga naye,'' aliiambia BBC.

Alikutana na Yusuf wiki mbili baada ya kukutana na kundi hilo mjini Maiduguri na aliombwa na kiongozi wa Boko Haram kwenda Afghanistan, alisema.

''Nilikaa Afghanistan kwa miezi mitatu. Nilipewa mafunzo kama mtaalamu wa mabomu.''

Bwana Abubakar amesema alikuwa anatakiwa awape mafunzo watu watano baada ya kurejea Nigeria, lakini kwa kuwa hakupokea malipo yake alitoroka.

Amesema wakati wa kuibuka mwezi Julai wakati wapiganaji wa Boko Haram wakiwa na majambia na kuanzisha mashambulio katika vituo vya polisi maeneo mbalimbali ya kaskazini, yeye alikuwa gerezani mjini Yola.

Baada ya kundi hilo kudhibitiwa miili kadhaa iliyonyongwa ilikutwa katika mako makuu ya kundi hilo ikijumuisha kwa uchache wahubiri wa kikristo watatu na kamanda wa ngazi ya pili katika shughuli za kijeshi.

Mamia ya wanachama wa kundi hilo pia waliuawa wakati vikosi vya usalama vilipojibu mashambulizi yaliyopelekea kifo cha Yusuf aliyepigwa risasi baada ya kukamatwa.

Polisi wanasema Yusuf aliuawa katika ufyatuaji risasi wakati alipojaribu kutoroka. Lakini makundi ya kutetea haki za binadamu wanasema ilikuwa ni mauaji yaliyodhamiriwa.

Kundi hilo linasemekana kuwa lilikuwa linapambana dhidi ya elimu ya nchi za magharibi na kiliamini kuwa serikali ya Nigeria imeathiriwa na mawazo ya kimagharibi.

Kikundi hicho kilitaka kuona sheria ya kiislam inatumika nchini kote Nigeria.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA