TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Wednesday, September 2, 2009

Mama mzazi amtetea mwanaye Zitto Kabwe kuwa ni safi,hahongeki, hanunuliki

7:20 AM
Fidelis Butahe na Mussa Mkama

WAKATI hali ikiwa bado tete ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), mama mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Shida Salum jana ameibuka katika Uchaguzi wa Baraza la Wanawake (Bawacha) na kudai kuwa mwanaye, Zitto Kabwe sio fisadi kama inavyoelezwa na wafuasi mbalimbali wa Chadema.

Akizungumza mbele ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilibroad Slaa, mama huyo ambaye ni mwenyekiti wa wanawake walemavu taifa, alitamka wazi kuwa mwanaye ni msafi, hanunuliki, hahongeki wala hatoi rushwa hivyo tuhuma hizo dhidi yake sio za kweli.

Alimtahadharisha Dk Slaa kuwa makini na viongozi wa makao makuu ya Chama hicho akituhumu kwamba baadhi yao ni mafisadi.

“Mheshimwa Katibu mkuu nimeshakufuata sana nikakumabia iangalie ofisi yako ya makao makuu itakuharibia chama na uliniahidi kuwa utalishughulikia lakini matokeo yake ndio haya,”alisema Shida na kuongeza;

“Magazeti yanamtukana Zitto kuwa ni fisadi lakini mimi ninasema kuwa Zitto hawezi kupokea wala kutoa rushwa kwa sababu anajua nini maana ya demokrasia, Katibu inayokuangusha ni ofisi yako ya makao makuu ichunguze.”

Akijibu hoja ya mama Zitto, Dk Slaa alisema kuwa ni kweli suala hilo linawezekana lakini akasisitiza kuwa kama ni rushwa ndani ya ofisi yake hata Zitto naye anahusika kwa sababu ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama ambaye kikatiba ndiyo mtendaji mkubwa wa ofisi hiyo.

“Kwa kicheko, nimekuelewa mama Zitto lakini unapozungumza hivyo ina maana unamuweka na Zitto pia maana yeye ndio naibu wangu, Zitto ni mwanao mimi ni naibu wangu sasa sijui niamue vipi, lakini hayo yote tuyaache mimi kama Katibu nitayafanyia kazi kwani tuliahidiana kutooneana haya wala kulindana hata kama mhusika anazungumza sana Bungeni,” alisema Slaa na kuongeza.

“Ninaposema kuwa chama kimeingiliwa na mafisadi sina maana kuwa Zitto ndiyo fisadi bali nawalenga wale wote wenye tabia ya kifisadi ndani ya chama pamoja na wale wanaotoka nje ya chama na kuleta ufisadi wao ndani ya chama.”

Awali akifungua Mkutano huo wa (Bawacha), Slaa alisema kuwa amepata ujumbe mfupi wa maneno kutoka kwa wajumbe kupitia simu yake ya mkononi kuwa kuna wagombea wamepenyeza rushwa kwa baadhi ya wajumbe ili waweze kuchaguliwa na kuwaonya kuwa wakigundulika watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria.

“Kutokana na hili nitaleta maofisa kutoka Takukuru ili wapambane na vitendo hivi vya rushwa kwa sababu moja ya vita kubwa ya Chadema ni rushwa, nitafanya hivi kwa kulinda demokrasia ndani ya chama atakayeshikwa na Takukuru shauri yake” alisema Slaa na kuongeza

“Mimi pamoja na wenzangu tumewataja walaji rushwa ndani ya serikali hatuwezi kushindwa kuwataja na kuwachukulia hatua wale wote wanaoendekeza rushwa ndani ya chama chetu, lakini pia ninawaonya wale wote wanaosema Slaa na Mbowe wanakula rushwa asimame na asema tena akiwa na ushahidi.”

Slaa akizungumza kwa jazba aliwataja maadui watatu wa Chadema kuwa ni Usalama wa taifa, Chama cha Mapinduzi(CCM) pamoja na vyombo vya habari vinavyotumiwa na mafisadi.

“Usalama wa taifa kuna gazeti moja wanalitumia kwa ajili ya kuichafua Chadema tunalijua, lakini pia lipo gazeti ambalo mimi mwenyewe nilimtaja mmiliki wa gazeti hilo kuwa ni fisadi Septemba 15 mwaka 2007 kwa hiyo sikushangaa lilivyoanza kuniandika vibaya kwa hiyo na hili linatumiwa,” alisema Slaa na kuongeza



0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA