TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Thursday, September 24, 2009

Akina Mramba washikilia msimamo wa kutofichua mashahidi wao

11:43 PM

Kesi ya matumizi mabaya ya madaraka inayowakabili mawaziri wa zamani wa wizara ya Fedha, Bazil Mramba na Daniel Yona pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Gray Mgonja imeendelea leo mahakamani, huku upande wa utetezi ukishikilia msimamo wake wa kugoma kutaja mashahidi wa upande wao.

Wakili wa Mramba Bw. Herbert Nyange leo ameendelea kutetea hoja ya kutotaja mashahidi wa upande wa utetezi kwa madai kuwa washtakiwa walikuwa ni watumishi wa Serikali na hivi sasa ni wastaafu hivyo hawawezi kutoa vitisho kwa mashahidi wa upande wa Serikali ambao ni watumishi.

Akasema hali hiyo ni tofauti kwa upande wa mashtaka ambapo Serikali kama chombo cha dola kinahodhi vyombo vya nguvu, hivyo inaweza kuwatolea vitisho mashahidi wa upande wa utetezi endapo itawataja hivi sasa.

Pia akasema mashahidi wengi waliotajwa kwa upande wa Serikali ni watumishi na wakati huo huo kesi inaihusu Serikali.

Wakili Nyange amesema ikiwa washtakiwa watakuwa na mashahidi ambao pia ni watumishi wa Serikali pia inaweza kuwa tatizo.

Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, kesi hiyo ilikuwa ikiendelea kurindima mahakamani hapo chini ya jopo la mahakimu watatu, wakiongozwa na Hakimu John Mtamwa.

Mramba na wenzake wanakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya madaraka kwa kutoa msamaha wa kodi kwa kampuni ya Alex Stewart na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Shilingi Bilioni 11.7.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA