
Leon Bahati na Exuper Kachenje
SIKU chache baada ya Halmashauri Kuu ya CCM (Nec) kuwaonya wanachama wanaopambana na mafisadi hadharani, wabunge kadhaa wa chama hicho wamesema hawatasalimu amri na badala yake wataendelea kupinga ufisadi popote bila kujali onyo hilo.
Wakati wabunge hao wakiitunishia misuli Nec, Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk Milton Makongoro Mahanga amefurahia uamuzi wa Nec akisema umetolewa kwa kadri alivyotarajia.
Wakizungumza na Mwananchi wabunge ambao wamekuwa wakitoa tuhuma mbalimbali za ufisadi ndani na nje ya Bunge walisema wataendelea 'kufa' na mafisadi na kwamba tamko hilo kamwe haliwezi kuwatisha.
Nec ilitoa tamko Agosti 17 mwaka huu baada ya kumaliza kikao chake mjini Dodoma, ikipiga marufuku viongozi na wanachama wake kuishambulia serikali bungeni, ikidai kuwa vita ya ufisadi ni ya chama na si ya kikundi cha watu wachache ndani ya chama hicho. Nec iliunda timu ya watu watatu kuwafuatilia wabunge wenye tabia hiyo.
Mkutano huo pia ulimweka kitimoto spika wa Bunge, Samuel Sitta huku wajumbe wakitaka anyang'anywe kadi yake ya uanachama kwa madai kuwa ana ruhusu na kushabikia mijadala inayoiweka serikali kwenye hali ngumu.Endeleea................
0 comments:
Post a Comment