Hakuna msimu wa ligi kuu ya Uingereza ambapo watu wamekuwa na shauku kubwa juu ya nini mameneja watazifanyia timu zao kama msimu huu. Bila shaka ndani ya kipindi cha miezi 10 ijayo mazungumzo mengi yatakuwa ni kuhusu mskotish (Alex Ferguson), muitaliano Carlo Ancelloti, muhispania Rafa Benitez, mfaransa Arsene Wenger na raia wa Wales Mark Hughes.
Katika kipindi chote hicho mameneja hao watakua kikaangoni, swali ni je ? nani atakuwa lawamani mwisho wa msimu ?. ni vigumu kupata jibu la haraka la swali hilo , kwani kama waswahili wasemavyo mpira hudunda, tuvute subira bila shaka tutajua zaidi ya hapo kuwa nani atashangilia, nani atakuwa kwenye lawama au pengine nani atafungasha virago ?
Hii inatokana na ule usemi maarufu wa kingereza usemao "managers are hired to be fired" na hii mara nyingi ni pale mambo yanapoenda ndivyo sivyo ndani ya klabu. Hatuna haja ya kurejea mifano ya hili kwani mashabiki wengi wako dhahiri nalo swala hili.
Labda maswali ambayo yanasumbua vichwa vya wengi hasa wapenda soka , kwa sasa ikiwa ni masaa machache yamebakia kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza ni kama yafuatayo .
Je ? ndoto ya Wenger kuwa vijana wake wadogo wataweza kukomaa kwa haraka na kuleta upinzani na maajabu ya soka katika ligi hiyo itatimia ?
Je ? mskotish Alex Ferguson ataweza kundeleza moto wa timu yake baada ya kuwapoteza Cristiano Ronaldo na Carlos Tevez ?
Usajili wa Glen Johnson na Alberto Aquilani utawasaidia vijogoo wa liverpool baada ya kuondoka kwa Alonso na Albeloa ? je? kocha wa timu hiyo muhispania Rafa Benitez ataendeleza makali yake ya msimu uliopita ?
Je ? kikosi ambacho kinawazoefu wengi waliokaa kwa muda kama timu (Chelsea) chini ya muitaliano Carlo Ancelloti kitafanikiwa kunyakua kikombe hicho ?
Je ? Mark Hughes meneja aliyetumia pesa nyingi zaidi kwa Usajili nchini Uingereza , atapata mafanikio yanayotarajiwa na wengi ? na kubwa zaidi ni nani atamuachia nafasi kocha huyo kwenye orodha ya klabu kubwa nne , yani Big Fours ?
0 comments:
Post a Comment