TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Tuesday, August 18, 2009

Nchi gani itamkaribisha Bemba?

8:42 AM

Hakuna nchi yoyote ikiwa ni pamoja na Uholanzi ambayo imejitolea kumpokea aliyekuwa makamu wa rais wa DRC, Jean Pierre Bemba ambaye aliwachiliwa kwa masharti na Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu, ICC.

Mahakama ya The Hague ipo nchini Uholanzi.

Mahakama hiyo ilikuwa imeziomba nchi saba za Uholanzi, Ubelgiji, Ureno, Ufaransa, Ujerumani, Italia na Afrika Kusini kumpokea bwana Bemba.

Anakabiliwa na mashtaka ya kuchochea mapigano katika nchi jirani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR.

Hata hivyo mahakama hiyo, imesema kwamba hataachiliwa hadi itakapoamuliwa ni nchi gani itakayompa makazi.

Baada ya kuachiwa kwa masharti wiki iliyopita na ICC, nchi nne Ufaransa, Uholanzi, Ubelgiji na Ureno zimemkataa Bemba.

Nchi zilizosalia Ujerumani, Italia na Afrika Kusini bado hazijatamka lolote iwapo zitamkubali au kumpa kisogo Bwana Bemba.

Hamu kubwa

Haijajulikana ni masharti aina gani ambayo Bwana Bemba atawekewa na mahakama hiyo.

Aidha katibu mtendaji wa chama chake cha MLC Thomas Luhaka ameiambia Idhaa ya Kiswahili ya BBC kwamba huenda akahitajika kutojihusisha na siasa.

Bwana Luhaka alisema wanachama wa MLC wana hamu kubwa ya kumpokea kiongozi wao.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA