NA MOHAMMED ISSA
MADIWANI wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala wamemchagua Jerry Slaa, kuwa Naibu Meya.
Slaa, ambaye ni Diwani wa kata ya Ukonga hakuwa na mpinzani katika kinyang'anyiro hicho.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Gabriel Fuime, alimtangaza Slaa kuwa Naibu Meya baada ya kupata kura zote 24, zilizopigwa na madiwani juzi, katika kikao cha Baraza la Madiwani.
Fuime alisema Slaa hana mpizani baada ya vyama vingine vya siasa kutowasilisha majina ya wagombea wa nafasi hiyo, hivyo kumfanya Slaa wa CCM kuchaguliwa.
Akizungumza baada ya kuchaguliwa, Slaa aliwashukuru madiwani wenzake kwa kumchagua na kuahidi kushirikiana nao ili kuhakikisha wanafanya kazi ya kuwaletea maendeleo wananchi.
"Nitafanya kazi kwa misingi ya sheria na naamini kwa kushirikiana na viongozi wengine wa halmashauri tutafanya mazuri, ambayo yatakuwa na faida kwa wananchi wa halmashauri hii," alisema Slaa.
Slaa ameshika wadhifa wadhifa huo baada ya aliyekuwa Naibu Meya, Kaselo Jaluo kumaliza muda wake. Uchaguzi wa Naibu Meya hufanyika kila baada ya mwaka mmoja.
0 comments:
Post a Comment