TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Friday, August 21, 2009

Mlipuaji mabomu Lockerbie awasili Libya

3:09 PM

Raia wa Libya aliyekuwa gerezani Scotland kwa kupatikana na hatia ya kulipua ndege ya Marekani huko Lockerbie mwaka 1988, amewasili Libya baada ya kuachiliwa huru.

Serikali ya Scotland ilimwachia Abdelbaset Ali al-Megrahi mwenye umri wa miaka 57 na mwenye ugonjwa wa saratani ya kibofu, kwa misingi ya huruma.

Rais wa Marekani Barack Obama amesema hatua hiyo ilikuwa ni ''kosa'', na jamaa wa waathirika wa Marekani wamechukizwa na uamuzi huo.

Wengi wa watu 270 waliokufa katika ulipuaji wa ndege hiyo walikuwa ni Wamerekani.

Katika mahojiano ya radio, Rais Obama amesema: ''Tumekuwa katika mawasilano na serikali ya Scotland, tukionyesha kuwa tunapinga hili. Tunadhani ilikuwa ni makosa kumwachilia.''

Ameongeza kuwa utawala wake umeiambia serikali ya Libya kuwa Megrahi hatakiwi kupewa mapokezi ya kishujaa na anatakiwa awekwe katika kifungo cha nyumbani.

Rana Jawad wa BBC mjini Tripoli anasema, ingawaje serikali ya Libya haijasema lolote kuhusu kuachiliwa huko, wataliona jambo hili ni kama ushindi wa kidiplomasia.

Mapema Alhamis polisi walimchukua Megrahi kutoka gereza la Greenock Scotland alimokuwa amefungwa tokea mwaka 2001, hadi uwanja wa ndege wa Glasgow kupanda ndege kuelekea Tripoli Libya.

Serikali ya Scotland imesema ilifanya mashauriano ya kina kabla ya Waziri wake wa Sheria Kenny MacAskill kufanya uamuzi huo, kufuatia maombi ya Megrahi ya kuachiwa kwa sababu za kibinadamu au kuhamishiwa katika gereza la Libya.

Aliviambia vyombo vya habari siku ya Alhamis kuwa ametupilia mbali maombi ya kuhamishwa kwa mfungwa.

Hata hivyo ushauri wa kidaktari ulikuwa unaonyesha kuwa Megrahi anategemewa kuwa amebakiza muda wa miezi mitatu tu kuishi.

Waziri huyo alitupilia mbali uchaguzi wa kumruhusu Megrahi kuishi nchini Scotland kwasababu za kiusalama.

Na Bwana MacAskill alisisitiza kuwa anaunga mkono adhabu ya kutiwa hatiani na hukumu ambayo ilitolewa kwa Megrahi.

''Bwana al-Megrahi hakuonyesha huruma yoyote wala faraja kwa waathirika wake. Hawakupewa nafasi ya kurudi na kuaga familia zao, achilia mbali siku za kufa kwao. Hakuna huruma aliyoionyesha kwao,'' alisema.

''Lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya sisi kumnyima huruma yeye na familia yake katika siku zake za mwisho.''

Bwana MacAskill aliendelea: ''Mfumo wetu wa sheria unataka hukumu itolewe, lakini huruma pia inapatikana.''

''Kwasababu hizi pekee, ni uamuzi wangu kuwa Mr Abdelbaset Ali Mohmed Al-Megrahi, aliyepatikana na hatia mwaka 2001 kwa ulipuaji mabomu ya Lockerbie, ambaye kwasasa anasumbuliwa na saratani ya kibofu, aachiwe huru kwasababu za huruma na aruhusiwe kurudi na kufia Libya.''

Bwana MacAskill amekuwa katika shinikizo kutoka Marekani kumshikilia gerezani Bwana Megrahi, huku Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton akisema kuachiliwa kwake ni makosa kabisa.''

''Huruma inahusu kushika imani inayotuwezesha kuishi, na kuwa wakweli katika thamani ya kibinadamu, bila kujali ni ukatili mkubwa kiasi gani uliofanywa,'' aliongeza.

Katika taarifa iliyotolewa baada ya kutoka katika gereza la Greenpck, Megrahi aliendelea kutetea kutokuwa na hatia.

Amesema: ''Ziku zilizobaki za maisha yangu zingali katika kivuli cha makosa ya kutiwa kwangu hatiani.

''Nimekabiliana na uchaguzi mgumu: kujitolea kufia gerezani kwa matumaini kwamba jina langu litaondolewa hatia au kurudi nyumbani
nikiwa nimebeba uzito wa hatia ya hukumu ambayo kamwe haitaondolewa.

''Uamuzi niliofanya ni kutokana na huzuni, kukata tamaa na hasira, ambapo nahofia kamwe sitaweza kumudu.''

Akizungumzia uamuzi huo katibu wa habari wa Ikulu ya Marekani Robert Gibbs amesema: ''Marekani inamasikitiko makubwa kwa uamuzi wa serikali ya Scotland kumwachia Abdel Basset Mohamed al-Megrahi.

''Kama tulivyokwishasema mara kwa mara kwa serikali ya Uingereza na Scotland, bado tunaendelea kuamini kuwa Megrahi anatakiwa kutumikia adhabu yake Scotland.''

Megrahi alipatikana na hatia ya mauaji ya kukusudia mwezi Januari mwaka 2001 katika kesi iliyoendeshwa chini ya sheria za Scotland nchini Uholanzi.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA