TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Wednesday, August 12, 2009

JK awapandisha vyeo majenerali watano JWTZ

10:35 PM

Rais Jakaya Kikwete, amewapandisha cheo maofisa wakuu watano wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kutoka cheo cha Brigedia Jenerali na kuwa Meja Jenerali kuanzia Julai 31, mwaka huu.

Taarifa ya Idara ya Habari na Uhusiano Makao Makuu ya JWTZ, jijini Dar es Salaam, iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana iliwataja waliopandishwa cheo, kuwa ni pamoja na Brigedia Jenerali Said Shaban Omar, ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Wanamaji na Brigedia Jenerali Charles Lawrence Makakala (Mkuu wa Sekretarieti ya Mipango na Maendeleo Jeshini).

Wengine, ni Brigedia Jenerali Festo Ndewilo Ulomi (Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Anga), Brigedia Jenerali Yodan Mtalima Kohi (Mkuu wa Tawi la Tiba Jeshini) na Brigedia Jenerali Salum Suleiman Salim (Mkuu wa Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo).

“Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatoa taarifa kwa vyombo vya habari na umma kuwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewapandisha cheo Maafisa Wakuu watano kutoka cheo cha Brigedia Jenerali na kuwa Meja Jenerali kuanzia tarehe 31 Julai 2009,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange atawavisha cheo kipya maaafisa hao leo Makao Makuu ya Jeshi, Upanga, Jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Rais Kikwete

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA