Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema lazima kufanyike uchunguzi kuhusu "adhabu ya jumla" waliyofanyiwa raia wa Mandera.
Shirika hilo lenye makao yake makuu nchini Marekani limesema utafiti wake umeonyesha kuwa maelfu ya watu waliteswa na wanawake kubakwa.
Lakini msemaji wa polisi Eric Kiraithe ameieleza BBC kuwa hapakutokea vitendo vya ubakaji wala watu kupigwa, badala yake aliitaka HRW kutoa ushahidi kuthibitisha madai yao.
"Hakika kuna ulazima wa kuangalia sheria za nchi zinazotoa fursa kwa mtu yoyote kuchapisha uongo kuhusu majeshi yetu ya usalama," alizungumza kupitia matangazo ya BBC asubuhi.
Awali mwaka huu, mchunguzi wa Umoja wa Mataifa alitoa madai kuhusu mauaji ya aina hiyo kwingineko nchini Kenya, Philip Alston, alisema polisi walijichukuliwa sheria mkononi.
0 comments:
Post a Comment