................................................................................................
MAKAMU
Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula amekifananisha chama cha
CHADEMA sawa na wachuuzi wa biashara za mkononi (wamachinga) kwa
kutokuwa na maeneo rasmi ya kuendesha shughuli zao.Mangula
amesisitiza kuwa CCM imejipanga na ina uhakika wa kushinda uchaguzi
mdogo wa ubunge wa jimbo la Kalenga wilaya ya Iringa vijijini.Kiongozi
huyo wa juu wa CCM aliyasema hayo jana katika kijiji cha Mugama kata ya
Mugama wilayani humo wakati akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu
ya CCM ya kata hiyo.
Mangula alitoa kauli hiyo baada ya kupokea taarifa ya maandalizi ya uchaguzi huo katika kata ya Mugama ambapo Katibu wa CCM kata
ya Mugama Sylvester Samon kueleza kuwa chama cha CHADEMA ambacho ni
mshindani wa CCM katika uchaguzi huo hakina dalili kushinda.
Samson
alisema CHADEMA haina ofisi hata moja katika kata nzima ya Mugama jambo
linalokitia hofu chama hicho na kulazimika kutumia mbinu chafu ikiwemo kushusha bendera za CCM na kuchana mabango ya mgombea wake. Baada
ya kuelezwa hayo, Mangula alisema CHADEMA kimekosa mwelekeo ndani ya
kata hiyo na jimbo zima la Kalenga kwa kuwa kimekuwa sawa na wamachinga kwa kutokuwa na na ofisi ambazo ni dalili ya kukubalika na kuwa na wanachama kwenye eneo husika.
“CHADEMA
hakina hata ofisi moja katika kata nzima, hivi unaweza kusema kina
dhamira ya dhati ya kuleta maendeleo kwenye eneo hili au wanatakakuwalaghai na kuwarubuni wananchi,” alisema. Alisema
CCM imejipanga kupata ushindi wa kishindo kutokana na mafanikio na
utekelezaji wa ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2010 ambapo mambo mbalimbali ya maendeleo yamefanikiwa kutekelezwa.
Kwa
mujibu wa Mangula, uchaguzi huo ni wa kujaza nafasi ya mbunge wa CCM
hivyo ni vyema wana-Kalenga wakamrudisha mwana-CCM ili akamilishe ahadi
zilizotolewa na Chama katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010. Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa CCM kata ya Mugama, Betha Luhavi, alisema
Chama kina taarifa kamili kuhusu wapiga kura wa eneo hilo hivyo hakuna mtu kutoka nje ya eneo hilo atakayepewa nafasi ya kujipenyeza ili kuvuruga uchaguzi huo.
Betha
alisema hadi sasa tayari CCM imefanikiwa kuyazunguukia matawi yote
yaliyo kwenye kata hiyo kwa lengo la kuhamasisha makada na wapenzi wake siku ya kupiga kura wajitokeze kupiga kura. Alisema
viongozi na wapenzi wa CCM watakuwa mstari wa mbele kuhamasisha amani
kipindi chote cha kamepeni na siku ya uchaguzi ili kuhakikisha ubnafanyika kwa amani. Aidha,
alisema CCM itashirikiana na vyombo vya dola kufichua uhalifu wa aina
yoyote unaolenga kuvuruga uchaguzi na amani katika kata hiyo na jimbo la Kalenga kwa jumla.
Uchaguzi
mdogo wa ubunge katika jimbo la Kalenga unatarajiwa kufanyika Machi 16,
mwaka huu ambapo CCM imemsimamisha Godfrey Mgimwa kuwa mgombea wake
atakaechuana na wagombea wengine. uchaguzi huo unafanyika kutokana na
kifo cha aliyekuwa mbunge wake Dk. William Mgimwa kufariki dunia Januari
mwaka huu wakati akipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini.
0 comments:
Post a Comment