Imeripotiwa kuwa mtu mmoja anayedaiwa kuwa alikuwa mume mtarajiwa (mchumba) wa Ufoo Saro aliyefahamika kwa jina la Ateri Mushi, amempiga risasi mwandishi wa habari na ripota wa ITV, Ufoo Saro na mama mazazi wa Ufoo Saro na kisha kujipiga risasi mwenyewe.
Akizungumza kwa njia ya simu, Steven Chuwa wa ITV amesema, katika tukio hilo limetokea kwenye nyumba alikokuwa akiishi mama wa Ufoo Saro, Kimbamba nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na kwamba Ufoo alikimbizwa katika hospitali ya Tumbi katika jitihada za kuuokoa uhai wake.
Baadaye taarifa zimesema kuwa Ufoo alihamishiwa kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Akizungumza na Ruben Mchome, Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Wambura amesema tukio hilo

limetokea majira ya alfajiri ya leo.
Mwanaume aliyefanya mauaji hayo alikuwa anafanya kazi kasika Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) nchini Sudan. Haijafahamika mapema bado kuwa alikuwa akifanya kazi gani wala katika kitengo gani.
Kamanda Wambura anasema inasemekana kulikua kuna ugomvi kati ya wawili hao ambapo walishindwa kuelewana na ndipo walipoamua kwenda kwa mama mzazi wa Ufoo Saro (mama mkwe). Alipofika huko inadaiwa kuwa mwanaume huyo alimshutumu mama mkwe wake kwamba anamtetea mwanaye (Ufoo Saro). Ndipo mwanaume huyo alipotoa bastola na kumpiga mama wa Ufoo Saro risasi kichwani na kumuua papo hapo na kisha akampiga Ufoo Saro risasi ya mbili, moja ya tumboni na nyingine mguuni. Inasadikiwa kuwa kwa kudhani kwamba amewaua wote, ndipo naye alipojifyatulia risasi kidevuni na kufariki dunia hapo hapo.
Kwa taarifa zaidi, tembelea MchomeBlog.com/Radio One

Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/10/mwandishi-habari-na-mtangazaji-itv-apigwa-risasi.html?utm_source=http%3A%2F%2Ffeeds.feedburner.com%2Fwavuti&utm_medium=feed&utm_campaign=Feed%3A+wavuti+%28Wavuti+%29#ixzz2hajhkf2p
0 comments:
Post a Comment