
Dk Kishiwa akiwa na mkewe, Mwajabu Chuma. Picha na Kalunde Jamal.
---
Huwezi kuamini lakini huu ndio ukweli, kwamba watu kadhaa wamekuwa wakimiminika kupata msaada wa tiba, ushauri wa kitabibu na wengine masomo ya udaktari kwa mtu ambaye imethibitika kwamba hivi sasa ana matatizo ya akili.
Huyu si mwingine bali ni Mark Paulo Kishiwa ambaye kitaaluma ni daktari, aliyewahi kufanya kazi Hospitali za Kasulu, mkoani Kigoma na Bugando mkoani Mwanza, lakini sasa mvua na jua humwishia akiwa maeneo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Ukimwona mara kadhaa utamkuta akiimba nyimbo zisizo rahisi kuzielewa kutokana na hali anayonekana kuwa nayo ya matatizo ya akili, lakini anapokuwa sawa, hugeuka kuwa msaada kwa wengi; madaktari wa MNH ambao huomba ushauri kwake, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi za Tiba Muhimbili (MUHAS) na wagonjwa ambao hutaka ushauri pia.Kwa habari zaidi bofya na Endelea............
0 comments:
Post a Comment