Kwanini ? Vibali vyote vya kuishi wageni visifutwe na kusajiliwa upya.
Msako lazima uwe na kasi kubwa tena uanzie mji mikubwa kama Dar,Arusha...
Kuanzia mwezi julai 2013 kiongozi mkuu wa nchi yetu rais Dk.Jakaya Kikwete katoka
agizo kuwa raia wote wa kigeni ambao ni wahamiaji haramu wamepewa siku 14,kuondoka au kujisalimisha katika vyombo vya dola.
Agizo
hili la rais lina lengo zuri tu kwa watanzania na usalama wa
watanzania,lakini utekelezwaji wake umekuwa hauna kasi,kwani idadi ya
wahamiaji haramu walio jisalimisha ni ndogo kulingana na waliopo
nchini,na kati ya hao walijisalimisha ni wahamiaji waliopo nje ya miji
mkubwa sio katika miji mikubwa kama Dar ,Arusha na
kwingineko !
Cha kushangaza kwamba kuna baadhi ya wahamiaji haramu au halali wanakiuka
kwa namna moja au nyingine sababu zinazowafanya kuwepo nchini Tanzania.
mfano raia wa kigeni aliyekuja nchini kwa kufanya kazi fulani na akapewa kibali
kwa ajili hiyo anakiuka kwa taratibu za uhamiaji na kuanza kuwa mfanyi biashara
ya
baa au dangulo fulani! au pengine kujiingiza katika biashara ambayo
mzawa anaweza kuifanya, na huku vyombo vya usalama vikimwangalia !
Hivi kuna uhalali wa kisheria Raia wa kigeni asiye na hata asili ya Tanzania kumiliki nyumba au Ardhi ?
Watanzania
wengi wamekuwa wakilalamika juu ya ongezeko la raia wa kigeni hususan
raia wa nchi za ulaya,Asia na nchi za kiarabu kumiliki au kununua
nyumba na ardhi nchini ,mfano wachina wanamiliki majumba au ardhi uenda
wakawa wanakiuka sheria fulani za nchi,na watanzania wanao wauzia nyumba
wageni hao nao pia wanajisaliti au kuisaliti nchi.
Ukiwikaji wa sheria za ajira ! mchina anapofanya ya kuuza duka na mitumba au kubeba zege ! Mzungu anapokuja kutalii na baadaye
kupata ajira ya muhudumu wa hotel ! hili nalo neno?
Bendi za muziki zinapo ajiri wanenguaji kutoka nje ya nchi!
Ndio maana watanzania walio wengi wanaona kuwa hipo haja kwa serikali
kuvifuta vibali vyote vya wageni na kuanza zoezi la kuvitoa upya na kuvihakiki
kwa kupitia Wizara ya mambo ya ndani.
Kama Rais JK kesha toa agizo tangu mwezi julai mbona utekelezaji wake
una mwendo wa pole ? wakati kiongozi mkuu wa nchi,ambaye ndiye amri
jeshi mkuu kishaagiza siku 14 tu kila muhamiaji haramu aondoke sasa
tena msako kwanini? usianze katika kutekeleza agizo la mkuu wa nchi.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Mbariki Rais JK
0 comments:
Post a Comment