TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Thursday, March 7, 2013

VIDEO – Mwananchi atwangwa risasi ya kifuani na askari Polisi

11:42 PM


Polisi mkoani Mtwara wameua raia mmoja kwa risasi baada ya kuzuka mapigano baina ya pande hizo mbili, mapigano ambayo yalitokana na hatua ya wananchi hao kuzuia gari ya mkuu wa wilaya wakishinikiza kulipwa kwa fedha zao za korosho wanazoidai serikali.
Kwa mujibu wa habari kutoka Mtwara, inaelezwa kuwa, wananchi hao baada ya kuweka magogo ya kuzuia msafara wa mkuu wa wilaya, Polisi walifika eneo la tukio na kuanza kurusha mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi hao, hatua ambayo iliwaudhi wananchi ambao walijibu mashambulizi kwa kutumia silaha za kijadi ikiwa ni pamoja na mishale.
Kutokana na hali hiyo, askari waliamua kutumia risasi za moto kupambana na hali hiyo, ambapo katika gatua hiyo, ndipo risasi moja ilimpata mwananchi aliyetambulishwa kwa jina la Said Mshamu, ambaye alikufa baada ya risasi kumpata kifuani
Chanzo:- jukwaa huru

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA