TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Saturday, March 2, 2013

Neno La Leo: Mengine Tuyafanyay​o Hupelekea Maanguko Yetu!

12:01 AM
Ndugu zangu,

Kupitia kitabu chake ’ Kusadikika’, mwanafasihi Shaaban Robert anamwelezea mchwa anayekaribia kufa.

Kwamba huota mbawa. Hukiacha kichuguu . Yumkini ataruka juu sana. Atakwenda mbali. Lakini, huko angani hufika mahali, mbawa hupukutika. Mchwa ataanguka chini. Mbali na kichuguu.

Hapo, mchwa hukabiriwa na hatari kubwa. Hawezi kuruka tena, na yu mbali na kichuguu. Na kichuguu ni taasisi. Hivyo, mchwa anaweza kuliwa na kinyonga, au hata chura. Na akinusurika na wawili hao, aweza kukanyagwa na unyayo wa mwanadamu, au hata tairi la baiskeli. Mchwa atakufa.

Naam, mengine tuyafanyayo hupelekea maanguko yetu. Hata kama mwanzoni huonekana kutupaisha juu angani.

” Nafikiri, ndio maana naishi”- Anasema mwanafalsafa Rene Descartes.

Na maarifa ya Sayansi yanatusaidia kuyabaini mahusiano kati ya dunia tunayoishi na mazingira yanayotuzunguka. Hiyo ni falsafa ya kivitendo. Ndio iliyo bora kuliko ile dhanifu- Speculative.

Iweje basi tumekuwa ni watu wa kuishi kwa dhahnia na hata kusambaza uvumi?

Tusisahau, kuwa kiu ya mwanadamu siku zote ni kutaka kuujua ukweli. Ukweli mzima.
Ni Neno La Leo.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA