Lugha ya blogaz na vyombo asilia vya habari zi tofauti. Wanahabari lakini ni watu waliosemea sawasawa kazi zao na kufuata utaratibu wa lugha, kusahihisha na kuhariri kazi. Bloga ni mtu yeyote tu mitaani au kijijini anayetaka kuelezea jambo.
[caption id="attachment_1655" align="aligncenter" width="500"]
Kitabu kipya cha Mwandishi nguli, Profesa Said Ahmed- Mhanga Nafsi Yangu- ambacho kinamwangalia mwanamke wa Kibongo anayekwenda kusoma ughaibuni. Kimetolewa na Sasa Sema (Longhorn) wa Kenya,2012. Ila tutathmini zaidi hilo... Blogu zilibuniwa kutangaza mambo na kadhia ambazo hazipo ndani ya vyombo habari mama na runinga. Zilibuniwa kumfaidisha mwananchi yeyote wa kawaida akibeba kamera na simu yake mkononi akaeleza habari za pale anapoishi. Hicho ndicho chanzo... Kama hukua na nafasi kuna Twitter ambayo ni fupi zaidi (maneno 30 tu!). Zana hizi ni muhimu sana kwa jamii ya leo. Hizi ni “habari za raia wa kawaida” . Umuhimu wa Blog, Twitter na You Tube umeonekana pale yalipotokea machafuko na harakati mbalimbali duniani kama Tunisia, Misri, Libya na Mashariki ya Kati nzima miaka miwili iliyopita. Dhoruba za mauaji ya mwanahabari Daudi Mwangosi zilisambaa dunia nzima haraka kutokana na uwezo huu muadhama. Nguzo zake ndizo hizo. Google ambaye hulipa matangazo ya biashara kutokana na “maudhui ya habari” husisitiza wanablogu na waandishi kuwa wa kweli na kutochezea kazi za wenzao. Kwetu Bongo hapana. Miaka ya karibuni makampuni makubwa makubwa na mabenki kama National Microfinance (NMB) yanasaidia kuwekezea wajisiria mali wadogo wadogo (yaani Blogaz). Mara nyingi makampuni haya hayaangalii kama wanablog hawa wananukuu kazi za wenzao, wanaandika mambo yao wenyewe au wanakopi tu na kubandika.
1 comments:
Maoni ya mwandishi Freddy Macha yakifanyiwa kazi lazima jamii ya mabloga itapiga hatua moja kwenda mbele...
Post a Comment