TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Thursday, August 9, 2012

Leo ni Hukumu ya Kesi Ya Aliyekuwa Balozi wa Tanzania, nchini Italia Profesa Costa Mahalu na Ofisa Utawala wa Ubalozi huo, Grace Martin.

2:03 PM
  Aliyekuwa Balozi wa Tanzania, nchini Italia Profesa Costa Mahal
--
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo inatarajia kutoa hukumu ya Kesi ya Uhujumu Uchumi na Kuisababishia Serikali hasara ya Euro 2 milioni, inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania, nchini Italia Profesa Costa Mahalu na Ofisa Utawala wa ubalozi huo, Grace Martin.

Profesa Mahalu na Martin wanakabiliwa na mashtaka sita yakiwamo ya uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya Euro 2,065,827.60, katika mchakato wa ununuzi wa jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Italia.

Hukumu ya kesi hiyo iliyokuwa ikinguruma mahakamani hapo kwa miaka kadhaa sasa, inatarajiwa kusomwa leo na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Ilvin Mugeta ambaye amekuwa akiisikiliza.

Awali, hukumu hiyo ilipangwa kusomwa Julai 11, mwaka huu lakini iliahirishwa kutokana na Hakimu Mugeta kukabiliwa na majukumu mengine. Kesi hiyo iliahirishwa na Hakimu Mkazi, Aloyce Katemana na kupanga kuwa hukumu hiyo itasomwa leo.

Kiongozi wa jopo la mawakili wa washtakiwa hao, Mabere Marando alisema jana kwamba anaamini kesi hiyo ambayo imechukua muda mrefu, leo inafikia mwisho kwa Mahakama kutoa hukumu.

Hata hivyo, hakutaka kuizungumzia kwa undani hukumu ya leo badala yake alisema kuwa wanachosubiri ni kuona itakavyokuwa, ila wako tayari kwa matokeo yoyote.“Sisi tunasubiri kuona hukumu ya Mahakama, kwani imekuwa ikisubiriwa sana. Kama akiachiwa tutafurahi na tutakunywa wine (mvinyo) usio na kilevi kama akifungwa basi tutapiga magoti kumwombea,” alisema Marando kwa utani huku akicheka.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA