Mlemvu
wa kutozungumza (bububu) akitumia haki yake ya kuchangia maoni yake
kupitia mkalimali wa kutafsiri lugha hiyo wakati akiwasilisha maoni yake
mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Tamzania, wakati ilipokuwa
ikikusanya maoni ya Wananchi wa Wilaya ya Chakechake Pemba.
Khamis
Said Abdalla (47) mkaazi wa shehia ya Madungu Chake chake, ambae ni
mlemavu akitumia haki yake ya kutowa maoni katika mchakato wa
kukusanya maoni ya Uandikwaji wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
wakati Tume hiyo ilipokuwa Kisiwani Pemba ikukusanya Maoni ya Wananchi
wa Mkoa wa Kusini Pemba, katika Wilaya ya Chakechake.
Mkaazi wa shehia ya Madungu Chake chake akitumia
haki yake ya kutowa maoni katika mchakato wa kukusanya maoni ya
Uandikwaji wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
wakati Tume hiyo ilipokuwa Kisiwani Pemba ikukusanya Maoni ya Wananchi
wa Mkoa wa Kusini Pemba, katika Wilaya ya Chakechake.
Wananchi wa Wilaya Chakechake Pemba wakinyosha mikono kupata nafasi ya
kutoa maoni yao kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Muungano wa
Tanzania wakiwa katika viwanja vya Tennis Chakechake.
0 comments:
Post a Comment