
002: Msaidizi
wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw Josephat Sura akiagana na Meneja Mahusiano
ya nje wa Vodacom Tanzania Bw. Salum Mwalim wakati Meneja huyo
alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh. Chiku Gallawa.

Mkuu wa
Mkoa wa Tanga Mh. Chiku Gallawa akizungumza na Meneja Mahusiano ya Nje
wa Vodacom Tanzania Bw. Salum Mwalim alipomtembelea ofisini kwake kwa
lengo la kusalimiana na kumpatia taarifa rasmi za hafla ya kufuturisha watoto yatima zaidi ya 500 inayoandaliwa na Vodacom Foundation jijini humo.

Meneja
Mahusiano ya Nje wa Vodacom Tanzania Bw. Salum Mwalim akizungumza moja
kwa moja na wakazi wa Mji wa Tanga na mikoa ya jirani kupitia kituo cha
Radio Mwambao FM kuhusu futari iliyoandaliwa na Vodacom Foundation kwa
watoto yatima zaidi ya 500 wa jijini Tanga leo Jumatano Julai 25, 2012.

Meneja
Uhusiano kwa Umma wa Vodacom Tanzania Bw. Matina Nkurlu akifafanua jambo
kwa Meneja wa Radio Mwambao FM ya Jijini Tanga Bw. Hashim Gulamwa
(Katikati) na Mkuu wa Vodacom Foundation Bw. Yessaya Mwakifulefule
wakati maofisa wa Vodacom walipotembelea kituo hicho leo Jumatano Julai
25, 2012 na kuzungumzia program ya Vodacom Foundation ya Ramadhan Care
& Share 2012 inayolenga kufuturisha watoto yatima sehemu mbalimbali
nchini wakati huu wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
--
Kampuni
ya Vodacom Tanzania leo inafuturisha zaidi ya watoto mia tano kutoka
madrasa za mjini na nje ya mji wa Tanga katika viwanja vya Ma-awal
Islamic ikiwa ni uzinduzi rasmi wa utaratibu wake wa kila wakati wa
mwezi mtukufu wa Ramadhan wa kujali na kuonesha upendo kwa watoto yatima
na makundi yasiyojiweza kwenye jamii – Ramadhan Care & Share
Futari
hiyo inayoandaliwa na Vodacom kupitia kitengo chake cha misaada kwa
jamii – Vodacom Foundation itahudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa
dini ya kiislamu na viongozi wa serikali mkoa wa Tanga
Mapema
jana Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mheshimiwa Chiku Gallawa alitoa baraka zake
kwenye futari hiyo alipotembelewa ofisini kwake na Meneja Mahusiano ya
Nje wa Vodacom Bw. Salum Mwalim na Meneja Mahusiano kwa Umma Bw. Matina
Nkurlu kwa lengo la kusalimiana.
“Utaratibu
wa kuwakumbuka yatima ni utaratibu mzuri nawapongeza Vodacom kwa upendo
wenu nasikitika sana kwamba sitokuwepo kama nilivyowaeleza wakati
mliponitumia ujumbe wa mualiko kwamba nitakuwa safarini Wilayani Handeni
kikazi, ila nawatakia kila la kheri na nitawakilishwa na Mkuu wa Wilaya
ya Tanga Mheshimiwa Halima Dendegu”Alisema Mh. Gallawa
Chini
ya utaratibu huo Vodacom Tanzania pia itafuturisha watoto yatima na
wa-Madrasa katika miji mbalimbali nchini sanjari na utoaji wa sadaka za
vyakula na vifaa vya shule kwa watoto hao.
0 comments:
Post a Comment