TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Thursday, July 26, 2012

Ngoma Africa band kupewa Award ya Kimataifa ! IDA-International Diaspora Award

8:40 PM
FFU Kuvuna walichopanda Ughaibuni!

Ngoma Africa band kupewa Tuzo la kimataifa,
" IDA - International Diaspora Award" 

Habari za uhakika zinatonya kuwa bendi maarufu ya muziki wa dansi
barani ulaya "The Ngoma Africa Band" au maarufu kwa jina la "FFU"
wazee wa virungu na makombora ya muziki,yenye makao yake
nchini Ujerumani, Bendi imetajwa kuwa ni bendi bora inayoitangaza miziki
ya Afrika kwa kasi duniani,na imechaguliwa kupewa tuzo maalumu la
" IDA - International Diaspora Award"  award hiyo inatolewa na
tahasisi za kimataifa,itakabidhiwa kwa kiongozi wa bendi hiyo Kamanda
Ras Makunja wa FFU siku ya Jumapili ya 12-8-2012 katika sherehe maalu za
Gala night zitakazo udhuriwa na wageni mbali mbali wakiwemo mastaa.
Inasemekana Sherehe za kukabidhiwa tuzo hiyo zitafanyika mjini Tubingen,
mkoa wa Baden württemberg, kusini mwa ujerumani.
Tahasisi za kimataifa zinazoshughulika na utamaduni wa kimataifa kuanzia
mwaka jana zilianza mkakati kutafuta bendi ya kiafrika inayolitangaza bara
la Afrika kwa kutumia muziki, na kuweka utaratibu wa kuzipigia kura bendi
hizo katika tovuti mbali mbali online na offline,Ngoma Africa Band ikajichulia
ushindi wa mamlioni ya kura, pia imegundulia kuwa bendi hiyo inakubalika na
 mamilioni  ya washabiki wa mataifa mbali mbali, 
Mzimu huo wa muziki kutoka Bongo unadaiwa kuwa na wafuasi milioni
50 duniani kote,hali hii inatishia maporomota wa muziki wa kimataifa,
kuwa FFU ni mali ya mamilioni ya washabiki,ni bendi ambayo kipenzi
cha mamilioni ya washabiki. katika kambi yao hii www.ngoma-africa.com
inakadiliwa kuwa na mamilioni ya lank.
Tunawatakia kila yaliyo mema FFU wetu www.ngoma-africa.com

1 comments:

Anonymous said...

Vichaa ffu kazi wanaiweza na wanamudu jukwaa

Post a Comment

 
BONYA HAPA