Juu Calvin
Muro akiwa katika amelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya
kujeruhiwa kwa risasi na askari wa kituo cha Polisi Mbezi kwa Yusuph
jijini Dar es Salaam juzi.Picha na Abdallah Khamis
---
DAR ES SALAAM, Tanzania
MKAZI
wa Mbezi kwa Yusuph Calvin Muro, amelazwa katika hospitali ya Taifa
Muhimbili baada ya kujeruhiwa na risasi zilizofyetuliwa na askari wa
jeshi la Polisi kituo cha Mbezi waliokuwa katika harakati za kulikamata lori lililobeba Mchanga.
Akiwa
kitandani katika hospitali hiyo ya Muhimbili, Muro alisema kuwa majira
ya saa moja na nusu usiku aliwaona polisi wakiwa katika gari
aina ya defenda wakilikimbiza lori la mchanga ambalo lilienda kupaki
katika eneo la kimara B na dereva wake kukimbilia katika gesti ya Pentagon kwa ajili ya kujisalimisha.
Aliongeza
kuwa askari waliokuwa wakimfukuza dereva huyo wa lori ambaye jina lake
halikufahamika, walienda hadi katika gesti ya pentagon na kumkamata
kisha wakaanza kumpiga kwa ngumi na teke
“Mwanzoni tulishangaa tukajua ni jambazi lakini tulipoona
wanaanza kumpiga kwa mangumi na mateke ikatufanya na sisi tusogee kujua
kinachoendelea ambapo tulimsikia yule dereva akilalamika kwa kusema
sina pesa na ninatakiwa nipeleke hesabu ninyi mmezoea kutuonea”alisema
Muro.
Alisema
baada ya wananchi kusikia kauli hiyo walianza kuwazomea maaskari ambao
waliondoka na baada ya muda wakarudi na kuanza kufyetua risasi hovyo na nyingine ndiyo ikampata chini ya makalio na kutokezea kwa mbele.
Sikuusikia
mlio wa risasi bali nilijihisi kama ninavuja maji na nilipojisogeza
katika mwanga nikaona tundu kubwa limejitokeza mbele ya paja langu huku
damu ikinivuja kwa wingi ndipo wenzangu waliponichukua na kunipeleka
Polisi kisha hospitali ya tumbi kibaha ambao nao walinihamishia hapa
Muhimbili majira ya saa nane usiku”aliongeza kusema Muro kwa taabu.
Aliongeza
kuwa baada ya kutembea kama hatua kumi huku wakiwa wamewasha indiketa
ya gari lao kuashiria wanaelekea kituo cha polisi Mbezi kwa Yusuph Mmoja
wao alielekeza bunduki upande wa gesti ya Pentagon na kisha kufyetua
bomu la machozi kabla ya wenzao kuanza kurusha risasi iliyompata Calvin
Muro.
“Hawa
wamezoea kukamata malori na kuchukua rushwa na huwa wana vizuizi vyao
tunawajua sasa katika hili yule dereva alikataa kusimama nao kwa hasira
wakaamua kumfuata na kumshushia kipigo”alieleza shuhuda huyo.
Mkuu wa Polisi wilaya ya Kimara aliyefahamika kwa jina moja la Papalika,alipoulizwa
kuhusiana na tuhuma za askari wake kutumia risasi kwa ajili ya
kulazimisha rushwa alikataa kutolea maelezo na kutaka atafutwe kamanda
wa Polisi mkoa wa Kinondoni.
“Msemaji
ni afande Kenyela mimi taratibu haziniruhusu kutolea maelezo hayo
unayoniuliza lakini kama askari wetu wanahusishwa na rushwa tutafanyia
kazi na ukweli utajulikana”alisema SP Paparika.
Jitihada za kumpata kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni zilishindikana baada ya namba zake ambazo ni O754 485911 na
0784 820033 kutopatikana hewani huku baadhi ya maaskari wakiahidi
kumueleza kupitia simu zao za redio kuwa anatafutwa na waandishi wa
habari. Askari hao walikuwa katika gari lenye namba za usajili Polisi PT 1412.
0 comments:
Post a Comment