Ni
baada ya kutambua mchango mkubwa uliofanywa na Bi Karrima Carter na
mwanawe Lukeman Carter wa Norrwich, Uingereza. Mtoto Luke baada ya kuona
picha za wanafunzi wa kijijini Mahango kwenye Mjengwablog aliamua
kutumia kazi ya project ya shuleni kwake kukusanya pesa kwa malengo
zifikie shilingi milioni moja za Kitanzania ili ziende kijijini Mahango
kusaidia kukarabati darasa la wanafunzi na chumba cha maktaba ya
wanafunzi pia. Mwitikio ukawa mkubwa kuliko alivyotarajia Luke na
wengine. Zikawa zaidi ya shilingi milioni moja na maboksi zaidi ya 35 ya
vifaa vya shule ikiwamo vifaa vya michezo pia.
Na
hapa nyumbani Tanzania kuna wengi wengine waliomuunga mkono Lukeman
Carter. Kupitia Mjengwa blog zimechangwa takribani shilingi milioni nne.
Na
kusafirisha maboksi hayo ya misaada iliyokusanywa na Lukeman na Bi
Karrima Carter kufika Tanzania ingekuwa ni gharama kubwa sana. Lakini,
Mtanzania, mzalendo Chris Lukosi na wenzake wa Serengeti Freighters And
Forwarders ama maarufu kama ' Wazee Wa Kazi' jana wamepokea mizigo hiyo
kutoka kwa Bi Karrima Carter na wamejitolea kusafirisha bure mizigo hiyo
ya misaada! Huo ni uzalendo uliokidhi viwango. Msaada huu utasaidia
kubadilisha maisha ya wengi Mahango na vijiji vya jirani kule Madibira,
Mbarali Mbeya. TUNAWASHUKURU SANA!
|
0 comments:
Post a Comment