TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Wednesday, June 20, 2012

“WAMILIKI WA JAMII FORUMS NI WATANZANIA WANAOITUMIA”-MAXENCE MELO (MAHOJIANO MAALUM) Read more: “WAMILIKI WA JAMII FORUMS NI WATANZANIA WANAOITUMIA”-MAXENCE MELO (MAHOJIANO MAALUM) - BongoCelebrity

10:10 AM
Tukiamua kubishana,tunaweza kufanya hivyo. Lakini endapo mwisho wa ubishi huo tutaamua kukubaliana,basi sina shaka kwamba sote tutakubaliana kwamba; miongoni mwa mitandao inayotembelewa na yenye ushawishi mkubwa na wa aina yake miongoni mwa watanzania wengi,mtandao wa Jamii Forums au kwa kifupi JF hauwezi kukosa katika orodha hiyo.
Lakini tofauti na mitandao mingine ambayo kimsingi imekuwa ikiendeshwa na mtu au watu wachache tu, JF ni mtandao unaondeshwa na watu wengi.Wengi wakiwa watanzania wenyewe. Pengine hiki ndicho kinachoufanya mtandao wa Jamii Forums kuwa na “upekee” kama nilivyogusia hapo juu.
Uendeshwaji huu wa jumla unafanyika kwa uhuru wa kila mtu kujiunga na kuanzisha mjadala,kuchangia au kuupanua zaidi.  Kimsingi,hivyo ndivyo mtandao wa Jamii Forums unavyochanja mbuga hivi leo. Wewe na mimi sote tunaweza kujiunga na kuendeleza mijadala. Ndani ya Jamii Forums kuna watu wa kila aina.Kuna watanzania.Kuna viongozi/wanasiasa,wanataaluma mbalimbali na pia kuna wenzangu na mie,watu wa kawaida wenye mapenzi na tekinolojia,habari,maarifa na wenye kutafuta mahali pa kutolea maoni yao huku wakiwa na imani kubwa kwamba kuna mtu atasoma ,kusikia na kuyafanyia kazi.
Ulianzaje? Nini malengo yake?Ni kweli kwamba mtandao huu unamilikiwa na chama fulani cha kisiasa? Mtandao huu una malengo gani?
Ili kupata majibu kwa maswali lukuki niliyokuwa nayo(na bila shaka uliyonayo wewe msomaji) nilimtafuta Maxence Melo Mubyazi(pichani), ambaye ni mwanzilishi-mwenza wa Jamii Forums na mtu ambaye mpaka hivi leo anabakia kuwa mhimili wa Jamii Forums ili kupata baadhi ya majibu kwa maswali yangu. Haya hapa ni mahojiano yangu naye;

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA