KAMPUNI ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania
imewatahadharisha wateja wao wa huduma
ya M-pesa kuwa makini kulinda namba zao
za siri zisifahamike na watu wengine,
kuepuka kuibiwa fedha zao.
Akizungunza na waandishi wa habari juzi ofisini kwake
Mlimani city Jijini Dar es salaam, afisa mawasiliano na mahusiano Joseline
Kamuhanda ameelezea madhara yatokanayo na kuvuja kwa namba za siri za mteja,
hali inayosababisha wizi.
“Ukweli mteja akitoa namba
ya siri kwa wakala ili amsaidie kumtolea pesa katika akaunti yake ni
hatari, kwa vile itategemea wakala huyo atakuwa na uadilifu wa kiasi gani,
lakini pia hata kwa mtu wa karibu kumpa kufahamu namba ya siri si jambo jema “ alisema
Kamuhanda.
Akizungunzia kuboreshwa kwa mtandao huo alisema M-pesa imezidi kuimarika baada ya
kuondoa tatizo la ‘network’ kusumbua wakati Fulani, hali ambayo ilileta
malalamiko kwa wateja.
“Tatizo la mtandao kusumbua katika zoezi utumaji pesa na
upokeaji halipo baada ya wataalam kulifanyia kazi kikamilifu na kuliondoa”
alisema Kamuhanda.
Akisisitiza kuhusiana na huduma za M-pesa afisa mkuu wa
biashara Dylan Lennox amewaomba wateja kuwa na utamaduni wa kutuza namba za
siri ikibidi kuzibadilisha kila baada ya muda, kuzuia hata ndugu wa karibu au
rafiki kuikariri namba hiyo.
“Kuna watu wapelelezi wa mambo anakuzoea inafikia kujua
namba ya siri ya akaunti yako, siku
unataka kutioa fedha katika
akaunti yako unaambiwa huna fedha za kutosha, badala yake unalaumu Vodacom
wamekuibia kitu ambacho si kweli” alisema Lennox.
Alisema tatizo la mteja kuibiwa linahusiana na yeye mwenyewe
kutoficha namba ya siri pengine kwa kutofahamu vyema namna ya njia za utoaji
fedha kwa njia ya M-pesa, bila kujua
huyo aliyempa namba ya siri ameikalili na kutumia kumuibia.
Lennox anamalizia kwa kusema
kuwa Voda com imejipanga vizuri zaidi kwa ajili ya kuwapa watanzania na
wateja wote kwa ujumla kuwapa huduma bora za kisasa ili kujiendeleza katika
masuala ya kiuchumi na kijamii na kuwaomba watanzania waitumie vizuri huduma
mpya ya wajanja.
Mwisho.
|
0 comments:
Post a Comment